Wednesday, 4 November 2015

MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)


MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)


Kiasi cha asilimia 2 ya mimba zote hutungwa nje ya mji wa uzazi. Hali hii hujuilikana kama ectopic pregnancy kwa kiingereza au extrauterine pregnancy kwa kitaalamu. Mara nyingi mimba zinazotunga nje ya kizazi huwa haziwezi kukua mpaka mwisho wa ujauzito, huweza kuleta hatari kwa afya ya mama hasa pale inapopasuka na kuvujisha damu tumboni mwa mama.

Namna Mimba Za Nje ya Kizazi Zinavyotokea

Kwa kawaida mbegu ya kiume na yai la kike hukutana katika mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na mimba hutungwa. Kiinitete husafri polepole kwenda kwenye mji wa uzazi ambako hujipandikiza kwenye ukuta wa uzazi na mimba huanza kukua. Katika ugonjwa huu wa mimba kuwa nje ya kizazi (ectopic pregnancy) mbegu ya kiume na yai huungana kutengeneza kiinitete. Badala ya kupandikizwa kwenye tumbo la uzazi, kiinitete huenda kujipandikiza sehemu nyingine tofauti na mji wa uzazi. Kinaweza kujipandikiza kwenye mirija ya uzazi, ovari, kwenye shingo ya uzazi na ndani ya tumbo (abdominal cavity). Mimba nyingi za nje ya kizazi hujipandikiza kwenye mirija ya uzazi ambapo huwa na hatari ya kupasuka kadri mimba inavyokua.
mimba nje ya kizazi (ectopic prgnancy)
mimba nje ya kizazi (ectopic prgnancy)
Mara chache sana mimba zinazotunga nje ya kizazi huweza kukua mpaka mwisho, nyingi huishia kupasuka na kuondolewa kwa upasuaji.

Sababu Hatarishi za Mimba Kutunga Nje ya Kizazi

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazochangia kutokea kwa mimba za nje ya kizazi.
Ingawa wakati mwingine zinazoweza kutokea bila sababu maalum kujulikana.

Dalili

Kufuatia wiki kadhaa baada ya kukosa siku zako za hedhi, unaweza kuanza kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kiuno, ambayo yanaweza kuwa upande mmoja. Maumivu yanaweza kuja na kuacha, kuwa makali sana kiasi cha kushindwa kuvumilia.
Hali hii inaambatana na kutokwa damu ukeni, mara nyingi ikitoka kidogo kidogo. Inaweza kuwa nyepesi au nzito nyeusi.
Wakati mwingine unaweza usipate dalili zozote, tatizo likagunduliwa wakati wa kipimo cha ultrasound. Kuna baadhi ya watu wanaweza wasipate dalili zozote na mimba kukua nje ya kizazi mpaka wakati wa kujifungua kukaribia.

Vipimo

Tatizo hili hugunduliwa kwa kipimo cha ujauzito (kwa mkojo au damu) kuthibisha kama mtu ana mimba na kisha ultrasound ya tumbo ili kuona mimba ilipo.
Kipimo cha mimba. Kipimo cha mimba cha mkojo (urinary pregnancy test) au cha mimba cha damu (serum HCG) hufanyika kuthibitisha uwepo wa mimba.
Ultrasound ya tumbo. Hii hufanyika kuonesha mimba ilipo. Wakati mwingine kwa wiki za mwanzoni (chini ya wiki 5) mimba iliyo nje ya kizazi inaweza kuwa ngumu kuiona kwenye ultrasound. Kama ipo nje ya kizazi au imepasuka itaonekana kwa kipimo hiki.

Matibabu

Matibabu ya mimba nje ya kizazi yanaweza kuwa ya dawa peke yake au kwa njia ya upasuaji. Matibabu ya dawa huanzishwa pale ambapo mimba ni ndogo na viwango vya hcg kwenye dami si vikubwa sana. Unaweza ukapewa dawa moja au mchanganyiko na ukawekwa kwenye ufuatiliaji wa karibu mpaka utakapopona.
Matibabu ya upasuaji hufanywa pale mimba inapopasuka, kuwa kubwa au mara chache imekomaa karibu na kujifungua. Upasuaji huusisha kuuondoa mimba iliyo nje ya uzazi, kama mirija imehusika basi kukata sehemu iliyoharibika na kuunganisha tena. Wakati mwingine mirija huondolewa moja kwa moja. Kwa mtoto ambaye ameshakomaa, tumbo hupasuliwa na mtoto kuondolewa.

Kupata Ujauzito Tena
Kwa wanawake wanaotarajia kupata tena ujauzito baada ya matibabu ya mimba kutunga nje ya uzazi, huweza kupata ujauzito wa kawaida. Ila kuna mambo matatu;
  • kupata mimba ya kawaida,
  • mimba kutunga tena nje ya kizazi au
  • kupata ugumba.
Kama uliwahi kupata mimba nje ya uzazi kabla ya hii, maambukizi kwenye mirija ya uzazi, upasuaji kwenye mirija ya uzazi au historia ya ugumba huongeza uwezekano wa tatizo kujirudia au kuwa mgumba.
Unaweza kupata ujauzito wa kawaida baada ya mimba kutunga nje ya kizazi. Zaidi ya asilimia 80 ya wanawake huenda kupata ujauzito wa kawaida baada ya kupona.


MAUMIVU YA MATITI

MAUMIVU YA MATITI

Maumivu ya matiti hutokea mara kwa mara kwa wanawake, hasa kwenye matiti yenyewe au karibu na kwapa. Hujulikana kwa kitaalamu kama mastalgia. Matiti au wengine wakiita maziwa, huweza kuuma yenyewe au kupata maumivu pale unapoyashika. Hali hii huwapa baadhi ya wanawake hofu wakidhani kuwa ni dalili ya saratani.
Maumivu ya matiti mara nyingi hutokea sehemu za juu za titi, wakati mwingine yakisambaa karibu na kwapa. Maumivu huwa ya kawaida, ingawa wakati mwingine yanaweza kuwa makkali kiasi cha kukufanywa ushindwe kufanya shughuli zako.
Maumi yanaweza kuwa kwenye ziwa moja au maziwa yote yakiambatana na kuvimba, uvimbe au mara chache kidonda. Pia yanaweza kujirudia kila mwezi.


Sababu Za Maumivu ya Matiti

Kuna sababu mbalimbali za maumivu  ya matiti zikiwemo;
  • Vivimbe kwenye matiti (fibrocystic changes). Matiti yanaweza kuwa na vivimbe visivyo saratani (cysts) ambavyo hujaa maji na kusababisha maumivu ya kujirudia rudia.
  • Premenstrual syndrome. Hali hii ni ya mabadiliko ya vichochezi vya uzazi ambavyo hujitokeza kabla ya hedhi kuanza. Husababisha matiti kujaa na kuuuma. Mumivu huwa makali zaidi siku 3 – 5 kabla ya hedhi na kupungua baada ya hedhi kuanza.
  • Maambukizi ya matiti (mastitis)
  • Usaa kwenyematiti (breast abscess)
  • Kutanuka kwa mirija ya maziwa (ductal ectasia)
  • Dawa kama digitalisaldactonemethyldopa
  • Kukoma kwa hedhi (menopause)
  • Saratani ya matiti. Ni aghalabu sana kwa saratani ya matiti kusababisha maumivu ya matiti.

Matibabu

Mara nyingi maumivu ya matiti huisha yenyewe baada ya muda fulani. Kukusaidia kupunguza maumivu ya matiti:
  • Vaa sidiria isiyokubana
  • Punguza unywaji wa chai na kahawa
  • Tumia vitamini E na mafuta ya primose
Kama unapata maumivu makali sana unaweza ukatumia dawa za maumivu kama paracetamolNSAIDs.
Vidonge vya majira hutumika kutibu maumivu yanayotokana na mabadiliko ya kihomoni.

JIANDAE KUPATA UJAUZITO

jiandae KUPATA UJAUZITO

Ujauzito wenye furaha, afya na amani ni matokeo ya maandalizi mazuri ambayo huanza kabla ya kushika mimba. Ni muhimu sana kujiandaa ili uweze kupata mtoto mwenye afya nzuri na wewe kufurahia ujauzito wako.


Vitu Muhimu Vya Kuzingatia Kabla ya Kupata Ujauzito
Kupata ujauzito wenye afya nzuri, ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo;
  • Fuata mtindo wa maisha unaojali afya yako vizuri. Hakikisha unapata chakula chenye virutubisho vya kutosha. Usisahau vyakula vya mboga mboga na matunda kwa wingikatika mlo wako.
  • Fanya mazoezi ya mwili angalau mara tano kwa wiki. Itaimarisha kinga yako ya mwili.
  • Unaweza kutumia vidonge vya virutubisho vya vitamini hasa vitamini B
  • Pima magonjwa ya zinaa na VVU. Ukiwa na magonjwa haya unaweza kumuathiri mtoto, hivyo pima na utibiwe kwanza.
  • Epuka unywaji wa pombe, kuvuta sigara au matumizi ya dawa za kulevya.
  • Epuka matumizi ya dawa kiholela
  • Jiandae kisaikolojia. Kupata mimba kutaleta mabadiliko kisaikolojia na majukumu ya ulezi ambayo ni muhimu ujiandae kisaikolojia kuyakabili.
  • Jiandae kiuchumi. Utahitaji matunzo mazuri, lishe bora, huduma za afya na kumlea mtoto utakayejifungua.

Kipindi Cha Kupata Ujauzito
Uwezekano wa kupata ujauzito huwa mkubwa kipindi ambacho yai la uzazi linatoka (ovulation). Hii huwa kwenye siku ya  10 mpaka 14 toka hedhi ilioanza (kama una mzunguko wa siku 28). kama mzunguko wako ni tofauti, chukua siku za mzunguko wako, kisha toa kwa 14. Siku utakayopata ndiyo yai la uzazi linatoka, hivyo kufanya mapenzi kuanzia siku 4 kabla na kuendelea kunaongeza uwezekano wa kupata mimba.

Je, Kuna Mitindo ya Mapenzi Inayosaidia Kupata Mimba?
Manii hufikia mirija ya uzazi ndani ya dakika chache bila kujali aina ya mtindo wa mapenzi. Hakuna mtindo maalumu utakaofanya upate mimba kwa haraka, yote ni sawa tu.

Nifanye Mapenzi Mara Ngapi Kupata Mimba?
Kukaa muda mrefu bila kukutana kimapenzi hupunguza uwezekano wa kupata mimba. Kufanya mapenzi kila siku 1 au mbili katika kipindi cha yai kutoka (fertile period) huongeza uwezekano wa kupata ujauzito.

Kuna Vyakula Vinavyoathiri Uzazi?
Ndiyo. Vyakula vya baharini vyenye madini ya zebaki (mercury) kwa wingi huathiri uzazi. Pia, vitu kama pombe na kunywa kahawa kwa wingi vinachangia kupunguza upatikanaji wa  mimba.

KUJUA JINSIA YA MTOTO WAKATI WA UJAUZITO

KUJUA JINSIA YA MTOTO WAKATI WA UJAUZITO

Ujauzito ni kipindi kinachoweza kuwa cha furaha hasa kwa wazazi watarajiwa. Katika kipindi hiki shauku kubwa huwa ni kujua mtoto atayezaliwa ni wa kike au kiume?


Je, inawezekana kujua jinsia ya mtoto wa wakati wa ujauzito?
Ndiyo inawezaka kujua jinsia ya mtoto wako wakati wa ujauzito. Via vya uzazi huwa vimekua na kuonesha tofauti kati ya vya kike na kiume wakati wa ujauzito wa miezi 4 na kuendelea.
Vipimo Gani Hutumika Kujua Jinsia ya Mtoto?
Mara nyingi kipimo cha Ultrasound hutumika katika kupima jinsia ya mtoto akiwa tumboni. Kwa kutumia ultrasound, viungo vya uzazi huonekana na kuwezesha kujua jinsia ya mtoto. Ultrasound inayofanyika kuanzia wiki ya 18 mpaka 20 huweza kuonesha jinsia ya mtoto. Wakati mwingine inaweza kutojulikana kama mtoto akiwa amelala vibaya.
Njia nyingine ya kujua jinsia ya mtoto ni kwa kutumia maji ya tumbo la uzazi (amniotic fluid). Maji haya huchukuliwa kwa njia ya sindano maalumu na kuchunguzwa kwa njia za kitaalamu.Hii hujulikana kama amniocentesis.

NAMNA YA KUWEZA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOITAKA.

NAMNA YA KUWEZA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOITAKA.
Mimi si mtaalam sana ila kutokana na mtu aliyeniuliza inbox nitajibu kwa jinsi ninavyoelewa mimi.
Ifahamike kuwa mbegu za kiume huishi si zaidi ya masaa matatu na huwa na mkia mrefu unaoziwesha kusafiri kwa haraka, na mbegu za kike huishi zaidi ya masaa 18 na huwa na mikia mifupi ambayo huzi fanya zisafiri polepole. Kwa hiyo tunatumia advantage hiyo kumpata mtoto wa jinsia tunayoitaka endapo utataka mtoto wa jinsia ya kiume unachotakiwa ni sex siku ya hatari(siku ambayo ovulation inafanyika kwa wanawake wenye mzunguko wa hedhi wa kawaida ni siku ya 14) mki sex siku hiyo kuna huwezekano mkubwa wa kupata
mtoto wa jinsia ya kiume kwasababu mbegu za kiume husafiri kwa haraka nakukutana na yai(ovu) na kutunga mimba. Ikiwa kama mtataka mtoto kike mnatakiwa kusex siku 1(au masaa zaidi 12) kabla ya siku ya hatari kwani mbegu za kike huishi kwa muda mrefu(na mbegu
za kiume zitakuwa zimekufa) kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kike.
Kwanza ni vizuri kumtanguliza mungu. Nadhani utakuwa umepata idea zakukusaidia nakutakia ndoa yenye furaha na upendo.

NJIA ZA KUPATA MTOTO WA KIUME AU WA KIKE

NJIA ZA KUPATA MTOTO WA KIUME AU WA KIKE

Watu wengi wamekuwa wakiwabebesha mzigo wanawake juu ya kupata mtoto wa kike au wa kiume na wengine kufikia kuwaacha wake zao eti kwaajili anazaa jinsia moja wakifikiri kuwa swala la kuzaa aina fulani ya mtoto ni lamwanamke peke yake wakati sio kweli mwanaume pia anachangia,sasa leo ningependa tujifunze jinsi ya kuchagua jinsia japo kuwa tunaamini kuwa Mungu pia anachangia ktk hili lkn kama tukifuata utaratibu pia inaweza kutusaidia sana.Mwanaume anamwaga shahawa au spamu kati ya milion 200 hadi 400,ambapo ndani yake kuna chromozomu X na Y.Kila yai la mwanamke lina chromozomu mbili za X. wakati manii ya mwanamume au spemu (yana chromozomu X na Y) kama chromozomu X ya mwanaume itarutubisha yai la mwanamke lenye X tupu, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamke.na endapo chromozomu Y ya mwanaume itarutubisha yai X la mwanamke atazaliwa mtoto wa kiume.Kwa kuwa chromozomu X ya mwanaume inaishi muda mrefu kuliko Y ukitaka kuzaa mtoto wa kike basi ujamiiane siku 2 au 3 kabla ya ovulation(ovulation ni kukomaa kwa yai ndani ya ovari ambalo litakuwa tayari kwa ajili ya kusubuli mbegu za kiume),lkn pia inashauriwa wanandoa wanapojamiiana basi mwanamke awe chini mwanaume juu kurahisisha spamu X kutunga mimba kwa urahisi,lakin pia njia ya kupata mtoto wa kiume ni kujamiiana masaa 12 baada ya ovulation.
Lakini sasa hivi kumekuwa na tatizo kubwa la watu kukosa kushika mimba wengine tangu alipoza zaa mtoto mmoja ndo basi na wengine hajapata kabisa hali hii imekuwa ikiongezeka kila siku kutokana na maisha tunayoishi,mazingira yetu na baadhi ya magonjwa ya uzazi napia low sperm count kwa wanaumejapo kuwa inawezekana kabisa tatizo hilo kuondoka na mtu akapata mtoto hata kama alikuwa amekata tamaa.
Kwa ushauri au tatizo lolote la kiafya tumia 0715448643 (unaweza kunifuata pia watsap

KUHARIBIKA KWA MIMBA KWA AKINAMAMA

Mimba kuharibika

Mimba iliyoharibika wiki sita hivi baada ya kutungwa, yaani wiki nane hivi baada ya hedhi ya mwisho.
Shamba la Mungu kwa watoto wasiozaliwa.
Mimba kuharibika ni tukio linalopatikana mara nyingi katika wanawake na mamalia wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wa mimba tumboni mwa mama.
Ni tukio tofauti na utoaji mimba ambalo linasababishwa na binadamu kwa makusudi.
Matukio yote mawili kwa kawaida yanaleta matatizo mbalimbali kwa mama.
Kuharibika kwa kijusi au kiinitete pengine kunatokana na mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile. Mimba nyingi huharibika kutokana na kutonakiliwa kisahihi kwa kromosomu; pia huweza kuharibika kutokana na mazingira.
Mimba inayotamatika kabla ya wiki ya 37 katika kipindi cha ujauzito husababisha uzaaji wa mtoto hai na hujulikana kama kuzaliwa mapema.
Kijusi akifa akiwa ndani ya chupa ya uzazi baada ya wiki 22, au wakati wa kujifungua, kwa kawaida hujulikana kama mzaliwa-mfu ausiriziki. Kuzaa mapema na uzazimfu kwa jumla hauchukuliwi kama kuharibika mimba ingawa matumizi ya maneno haya wakati mwingine yakaingiliana.
Kati ya 10% na 50% ya mimba hutamatishwa kwa njia zinazoweza kubainishwa kimatibabu, kutegemea umri na afya ya mwanamke mjamzito.
Mimba nyingi huharibika katika hatua za mapema sana za ujauzito, kiasi kwamba mwanamke hafahamu kwamba alikuwa mjamzito. Utafiti mmoja uliofanywa kupima homoni za kutoa yai na ujauzito uligundua kuwa 61.9% ya uhamili ulipotezwa kabla ya wiki 12, na 91.7% ya kuhabirika huko kulitokea bila ya dalili, na bila ya fahamu ya mwanamke aliyekuwa mjamzito. [1]
Hatari ya kutoka mimba ghafla hupungua kwa kiasi kikubwa baada ya wiki 10 kutoka kipindi cha mwisho cha hedhi[2]
Kisababishi kikuu cha mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza huwa matatizo ya kromosomu ya kiinitete / kijusi, [3]hali ambayo husababisha angalau 50% ya kutoka kwa mimba mapema. [4]
Sababu nyingine ni pamoja na magonjwa ya mishipa (kama lupus), kisukari, matatizo mengine ya homoni, maambukizi, na matatizo ya chupa ya uzazi. [3]
Umri mkubwa na historia ya mimba zilizotangulia kuharibika ni sababu mbili kuu zinazohusishwa kwa pakubwa na mimba kuharibika ghafla. [4]
Hiyo inaweza pia kusababishwa na kiwewe kinachotokana na ajali.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Jump up Edmonds DK, Lindsay KS, Miller JF, Williamson E, Wood PJ (1982). "Early embryonic mortality in women". Fertil. Steril. 38 (4): 447–453. PMID 7117572 .
  2. Jump up Nilsson, Lennart; Lars Hamberger [1965] (1990). A child is bornGarden City, New YorkDoubledayISBN 0-385-40085-3OCLC 21412111.
  3. ↑ Jump up to:3.0 3.1 Stöppler, Melissa Conrad; William C. Shiel, Jr., ed.. Miscarriage (Spontaneous Abortion)MedicineNet.com. Iliwekwa mnamo 2009-04-07.
  4. ↑ Jump up to:4.0 4.1 Jauniaux, E.; P. Kaminopetros and H. El-Rafaey (1999). "Early pregnancy loss", in Martin J. Whittle and C. H. Rodeck: Fetal medicine: basic science and clinical practice. Edinburgh: Churchill Livingstone, 837ISBN 0-443-05357-XOCLC 42792567.