Wednesday, 4 November 2015

MAUMIVU YA MATITI

MAUMIVU YA MATITI

Maumivu ya matiti hutokea mara kwa mara kwa wanawake, hasa kwenye matiti yenyewe au karibu na kwapa. Hujulikana kwa kitaalamu kama mastalgia. Matiti au wengine wakiita maziwa, huweza kuuma yenyewe au kupata maumivu pale unapoyashika. Hali hii huwapa baadhi ya wanawake hofu wakidhani kuwa ni dalili ya saratani.
Maumivu ya matiti mara nyingi hutokea sehemu za juu za titi, wakati mwingine yakisambaa karibu na kwapa. Maumivu huwa ya kawaida, ingawa wakati mwingine yanaweza kuwa makkali kiasi cha kukufanywa ushindwe kufanya shughuli zako.
Maumi yanaweza kuwa kwenye ziwa moja au maziwa yote yakiambatana na kuvimba, uvimbe au mara chache kidonda. Pia yanaweza kujirudia kila mwezi.


Sababu Za Maumivu ya Matiti

Kuna sababu mbalimbali za maumivu  ya matiti zikiwemo;
  • Vivimbe kwenye matiti (fibrocystic changes). Matiti yanaweza kuwa na vivimbe visivyo saratani (cysts) ambavyo hujaa maji na kusababisha maumivu ya kujirudia rudia.
  • Premenstrual syndrome. Hali hii ni ya mabadiliko ya vichochezi vya uzazi ambavyo hujitokeza kabla ya hedhi kuanza. Husababisha matiti kujaa na kuuuma. Mumivu huwa makali zaidi siku 3 – 5 kabla ya hedhi na kupungua baada ya hedhi kuanza.
  • Maambukizi ya matiti (mastitis)
  • Usaa kwenyematiti (breast abscess)
  • Kutanuka kwa mirija ya maziwa (ductal ectasia)
  • Dawa kama digitalisaldactonemethyldopa
  • Kukoma kwa hedhi (menopause)
  • Saratani ya matiti. Ni aghalabu sana kwa saratani ya matiti kusababisha maumivu ya matiti.

Matibabu

Mara nyingi maumivu ya matiti huisha yenyewe baada ya muda fulani. Kukusaidia kupunguza maumivu ya matiti:
  • Vaa sidiria isiyokubana
  • Punguza unywaji wa chai na kahawa
  • Tumia vitamini E na mafuta ya primose
Kama unapata maumivu makali sana unaweza ukatumia dawa za maumivu kama paracetamolNSAIDs.
Vidonge vya majira hutumika kutibu maumivu yanayotokana na mabadiliko ya kihomoni.

1 comment:

  1. Mimi mke wangu Anamiezi3 tangu awekewe kijiti cha uzazi wa mpango lakin chakushangaza tangu tar1 mwezi6 aliingia bleed hadi Leo bleed haikati japokuwa bleed yake ni matonematone lakin nashangaa hiv Leo tena amepatwa na maumivu makali ya matiti yani my stress zimenijaa naomben ushauri jamanii

    ReplyDelete