Mimba kuharibika
Mimba kuharibika ni tukio linalopatikana mara nyingi katika wanawake na mamalia wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wa mimba tumboni mwa mama.
Ni tukio tofauti na utoaji mimba ambalo linasababishwa na binadamu kwa makusudi.
Matukio yote mawili kwa kawaida yanaleta matatizo mbalimbali kwa mama.
Kuharibika kwa kijusi au kiinitete pengine kunatokana na mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile. Mimba nyingi huharibika kutokana na kutonakiliwa kisahihi kwa kromosomu; pia huweza kuharibika kutokana na mazingira.
Mimba inayotamatika kabla ya wiki ya 37 katika kipindi cha ujauzito husababisha uzaaji wa mtoto hai na hujulikana kama kuzaliwa mapema.
Kijusi akifa akiwa ndani ya chupa ya uzazi baada ya wiki 22, au wakati wa kujifungua, kwa kawaida hujulikana kama mzaliwa-mfu ausiriziki. Kuzaa mapema na uzazimfu kwa jumla hauchukuliwi kama kuharibika mimba ingawa matumizi ya maneno haya wakati mwingine yakaingiliana.
Kati ya 10% na 50% ya mimba hutamatishwa kwa njia zinazoweza kubainishwa kimatibabu, kutegemea umri na afya ya mwanamke mjamzito.
Mimba nyingi huharibika katika hatua za mapema sana za ujauzito, kiasi kwamba mwanamke hafahamu kwamba alikuwa mjamzito. Utafiti mmoja uliofanywa kupima homoni za kutoa yai na ujauzito uligundua kuwa 61.9% ya uhamili ulipotezwa kabla ya wiki 12, na 91.7% ya kuhabirika huko kulitokea bila ya dalili, na bila ya fahamu ya mwanamke aliyekuwa mjamzito. [1]
Hatari ya kutoka mimba ghafla hupungua kwa kiasi kikubwa baada ya wiki 10 kutoka kipindi cha mwisho cha hedhi. [2]
Kisababishi kikuu cha mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza huwa matatizo ya kromosomu ya kiinitete / kijusi, [3]hali ambayo husababisha angalau 50% ya kutoka kwa mimba mapema. [4]
Sababu nyingine ni pamoja na magonjwa ya mishipa (kama lupus), kisukari, matatizo mengine ya homoni, maambukizi, na matatizo ya chupa ya uzazi. [3]
Umri mkubwa na historia ya mimba zilizotangulia kuharibika ni sababu mbili kuu zinazohusishwa kwa pakubwa na mimba kuharibika ghafla. [4]
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Edmonds DK, Lindsay KS, Miller JF, Williamson E, Wood PJ (1982). "Early embryonic mortality in women". Fertil. Steril. 38 (4): 447–453. .
- ↑ Nilsson, Lennart; Lars Hamberger [1965] (1990). A child is born. Garden City, New York: Doubleday. ISBN 0-385-40085-3. OCLC 21412111.
- ↑ 3.03.1 Stöppler, Melissa Conrad; William C. Shiel, Jr., ed.. Miscarriage (Spontaneous Abortion). MedicineNet.com. Iliwekwa mnamo 2009-04-07.
- ↑ 4.04.1 Jauniaux, E.; P. Kaminopetros and H. El-Rafaey (1999). "Early pregnancy loss", in Martin J. Whittle and C. H. Rodeck: Fetal medicine: basic science and clinical practice. Edinburgh: Churchill Livingstone, 837. ISBN 0-443-05357-X. OCLC 42792567.
No comments:
Post a Comment