SIKU HATARI ZA KUBEBA MIMBA KWA WANAWAKE..
Moja ya makala zilizopita niliwahi kuongelea namna ya kupata mtoto wa kiume na jinsi ya kujua siku za mwanamke za hatari za kubeba mimba ni zipi lakini watu wengi wamekua wakinipigia simu kwamba hawakuelewa.
Leo ntarudia maada hii na naomba msomaji usome kwa makini sana.
Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.
Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao.
Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.
Je siku za hatari ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.
Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.
Kama mzunguko wako ni mrefu labda siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.
Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment