Wednesday, 4 November 2015

KUJUA JINSIA YA MTOTO WAKATI WA UJAUZITO

KUJUA JINSIA YA MTOTO WAKATI WA UJAUZITO

Ujauzito ni kipindi kinachoweza kuwa cha furaha hasa kwa wazazi watarajiwa. Katika kipindi hiki shauku kubwa huwa ni kujua mtoto atayezaliwa ni wa kike au kiume?


Je, inawezekana kujua jinsia ya mtoto wa wakati wa ujauzito?
Ndiyo inawezaka kujua jinsia ya mtoto wako wakati wa ujauzito. Via vya uzazi huwa vimekua na kuonesha tofauti kati ya vya kike na kiume wakati wa ujauzito wa miezi 4 na kuendelea.
Vipimo Gani Hutumika Kujua Jinsia ya Mtoto?
Mara nyingi kipimo cha Ultrasound hutumika katika kupima jinsia ya mtoto akiwa tumboni. Kwa kutumia ultrasound, viungo vya uzazi huonekana na kuwezesha kujua jinsia ya mtoto. Ultrasound inayofanyika kuanzia wiki ya 18 mpaka 20 huweza kuonesha jinsia ya mtoto. Wakati mwingine inaweza kutojulikana kama mtoto akiwa amelala vibaya.
Njia nyingine ya kujua jinsia ya mtoto ni kwa kutumia maji ya tumbo la uzazi (amniotic fluid). Maji haya huchukuliwa kwa njia ya sindano maalumu na kuchunguzwa kwa njia za kitaalamu.Hii hujulikana kama amniocentesis.

No comments:

Post a Comment