Wednesday 4 November 2015

JIANDAE KUPATA UJAUZITO

jiandae KUPATA UJAUZITO

Ujauzito wenye furaha, afya na amani ni matokeo ya maandalizi mazuri ambayo huanza kabla ya kushika mimba. Ni muhimu sana kujiandaa ili uweze kupata mtoto mwenye afya nzuri na wewe kufurahia ujauzito wako.


Vitu Muhimu Vya Kuzingatia Kabla ya Kupata Ujauzito
Kupata ujauzito wenye afya nzuri, ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo;
  • Fuata mtindo wa maisha unaojali afya yako vizuri. Hakikisha unapata chakula chenye virutubisho vya kutosha. Usisahau vyakula vya mboga mboga na matunda kwa wingikatika mlo wako.
  • Fanya mazoezi ya mwili angalau mara tano kwa wiki. Itaimarisha kinga yako ya mwili.
  • Unaweza kutumia vidonge vya virutubisho vya vitamini hasa vitamini B
  • Pima magonjwa ya zinaa na VVU. Ukiwa na magonjwa haya unaweza kumuathiri mtoto, hivyo pima na utibiwe kwanza.
  • Epuka unywaji wa pombe, kuvuta sigara au matumizi ya dawa za kulevya.
  • Epuka matumizi ya dawa kiholela
  • Jiandae kisaikolojia. Kupata mimba kutaleta mabadiliko kisaikolojia na majukumu ya ulezi ambayo ni muhimu ujiandae kisaikolojia kuyakabili.
  • Jiandae kiuchumi. Utahitaji matunzo mazuri, lishe bora, huduma za afya na kumlea mtoto utakayejifungua.

Kipindi Cha Kupata Ujauzito
Uwezekano wa kupata ujauzito huwa mkubwa kipindi ambacho yai la uzazi linatoka (ovulation). Hii huwa kwenye siku ya  10 mpaka 14 toka hedhi ilioanza (kama una mzunguko wa siku 28). kama mzunguko wako ni tofauti, chukua siku za mzunguko wako, kisha toa kwa 14. Siku utakayopata ndiyo yai la uzazi linatoka, hivyo kufanya mapenzi kuanzia siku 4 kabla na kuendelea kunaongeza uwezekano wa kupata mimba.

Je, Kuna Mitindo ya Mapenzi Inayosaidia Kupata Mimba?
Manii hufikia mirija ya uzazi ndani ya dakika chache bila kujali aina ya mtindo wa mapenzi. Hakuna mtindo maalumu utakaofanya upate mimba kwa haraka, yote ni sawa tu.

Nifanye Mapenzi Mara Ngapi Kupata Mimba?
Kukaa muda mrefu bila kukutana kimapenzi hupunguza uwezekano wa kupata mimba. Kufanya mapenzi kila siku 1 au mbili katika kipindi cha yai kutoka (fertile period) huongeza uwezekano wa kupata ujauzito.

Kuna Vyakula Vinavyoathiri Uzazi?
Ndiyo. Vyakula vya baharini vyenye madini ya zebaki (mercury) kwa wingi huathiri uzazi. Pia, vitu kama pombe na kunywa kahawa kwa wingi vinachangia kupunguza upatikanaji wa  mimba.

No comments:

Post a Comment