Saturday 21 November 2015

ZIJUE SABABU ZINAZOPELEKEA WANAWAKE WENGI KUTOKUSHIKA MIMBA

Mwanamke kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa mwanamke anayo historia kama alishawahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa au iliharibika.
Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita ‘infertility’ au ugumba.
Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.
Maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe na magonjwa sugu pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.

Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanamke
Vyanzo vya matatizo haya vinahusisha aina zote mbili za ugumba za ‘Primary’ na sekondari’. Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai ‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai.
Hii husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi, tutakuja kuona.

Katika makala zijazo
Dalili za upevushaji wa mayai zipo nyingi, tutakuja kuziona hapo baadaye lakini kubwa ni kwa mwanamke kupata ute wa uzazi ambapo upo wa aina tatu.
Pia upevushaji tunaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi unaweza kupata mimba.
Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni kwenye mirija, mirija inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au maji. Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi.
Utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija. Matatizo ya mirija husababisha ugumba kwa kiasi kikubwa ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.
Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi ambapo linatoka kwa nje badala kuwa ndani. Hali hii kitaalam inaitwa ‘Endometriosis’. Siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini linaathiri baadhi ya wanawake.
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo na huwa makali wakati wa hedhi na kusababisha damu ya hedhi kutoka kidogokidogo, mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.
Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambao humuathiri mwanamke. Mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri, anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa.
Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa hiyo ni vema naye akafanyiwa  uchunguzi endapo wanatafuta mtoto au ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.
Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina inaonekana mume hana tatizo wala mke hana tatizo, hali hii inaitwa kitaalamu ‘Unexplained Inferlity.  Kwa hiyo, ni vema uchunguzi wa kina ufanyike. Tatizo hili tutakuja kuliona katika makala zijazo.

Uchunguzi
Matatizo ya ugumba ni makubwa na huumiza vichwa vya watu wanaotafuta ujauzito. Tumeona sababu kuu za ugumba lakini mambo mengine  yanayohusiana na lishe na magonjwa sugu yanayoathiri uzazi. Tutakuja kuzungumzia.
Uchunguzi hufanyika kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa na wilaya. Vipimo mbalimbali hufanyika kama damu kuangalia viwango vya homoni, ultrasound na mirija uzazi.

SIKU HATARI ZA KUBEBA MIMBA KWA WANAWAKE..



                                                           
      
Moja ya makala zilizopita niliwahi kuongelea namna ya kupata mtoto wa kiume na jinsi ya kujua siku za mwanamke za hatari za kubeba mimba ni zipi lakini watu wengi wamekua wakinipigia simu kwamba hawakuelewa.
Leo ntarudia maada hii na naomba msomaji usome kwa makini sana.

Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.

Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao. 

Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka  sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.

Je siku za hatari ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba. 

Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku  28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.

Kama mzunguko wako ni mrefu labda  siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.

Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.

Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka  ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike.

                                               

MADHARA KUMI YA KUPIGA PUNYETO…..{ MASTURBATION}




Punyeto ni nini?
Hii ni tabia ambayo mwanamke au mwanaume anajichua sehemu za siri ili kufika kileleni, mara nyingi kitendo hiki hufanyika na muhusika akiwa peke yake chumbani au bafuni.
Wahanga wengi wa tabia hii ni wanaume kwani huanza katika umri mdogo sana kwasababu ya uoga wa kufuata wasichana na kuangalia video za ngono ambazo huwasukuma kufanya vitendo hivi..
Lakini punyeto huambatana na madhara makubwa ya kijamii na kiafya na leo tutaangalia madhara hayo kumi ya punyeto..


  1. 1.       Punyeto humfanya mtu awe mlegevu bila kua na nguvu kabisa mda wote kwani nguvu nyingi sana hutumika kwenye tendo hili.
  1. 2.       Ni moja ya chanzo kikuu cha kupoteza nguvu za kiume kwasababu ya kuharibu mishipa ya fahamu wakati mtu akijisugua.
  1. 3.       Punyeto hupunguza idadi ya mbegu za kiume{low sperm count} hivyo ni mbaya sana kwa wapenzi wanaotafuta mototo.
  1. 4.       Husababisha mtu kusahau sana na kushindwa kufanya vitu kwa makini zaidi.
  1. 5.       Humfanya mtu awe mchovu mda wote na kusinzia ovyo kila anapomaliza kupiga punyeto.
  1. 6.       Husababisha mwanaume kutoa mbegu haraka kipindi cha tendo la ndo na kushindwa kumfikisha mwanamke kileleni..{pre mature ejaculation}
  1. 7.       Husababisha msongo mkubwa wa mawazo kwani kila ukimaliza tendo hilo unajuta sana na kuapa kwamba hutarudia tena.
  1. 8.       Huleta utumwa wa kifikra kwani ukishaanza huwezi kuacha kirahisi{ addiction}
  1. 9.       Punyeto husababisha mwanaume au mwanamke kukosa hamu kabisa na mwenza wake hivyo kuleta usumbufu kwenye mahusiano.
  1. 0.   Punyeto ni chanzo kikuu cha ngono za jinsia moja shuleni na vyuoni ambazo huambukiza magonjwa ya zinaa kama kaswende, gono na ukimwi kirahisi sana.


Mwisho: acha punyeto na uanze maisha mapya kiakili, kimwili na kiroho na acha kusema hii ndio punyeto ya mwisho sitarudia tena,  acha mara moja…

                                    MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                                 
                                                STAY ALIVE 

                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

3 comments:

Anonymous said...
Hiii nzuriii
Ila jee ni njia zip sahihi za mtu alyekua adicted na punyeto kuweza kuacha
Kalegamye Hinyuye said...
nashukuru kwa swali lako..makala ijayo itaongelea jinsi ya kuacha punyeto. endelea kusoma blog hii uelimike zaidi.
Anonymous said...
Je mtu anapo acha mtindo huo vip nguvu zake uwa anarud kua fiti au ndo ivo ivo mpak mwisho?? Ebu tueleweshe man

MATIBABU YA NGUVU ZA KIUME KWA WAATHIRIKA WA PUNYETO…..



                                                                              

Karibuni ndugu wasomaji katika blog yetu ya siri za afya bora katika muendelezo huu wa makala za kutujenga kiafya..makala mbili zilizopita niliongelea kuhusu madhara na jinsi ya kuacha punyeto, nilipokea simu nyingi sana za watu waliokiri wameathirika sana na tatizo hilo na wakataka kujua jinsi gani wataondokana na adha hiyo… Wengine niliwapa ushauri tu na wengine niliwapa matibabu ya chakula, mazoezi na dawa na kwa sasa wananipigia na kukiri kwamba wameacha punyeto na kupona kabisa madhara ya kupungukiwa nguvu za kiume yaliokua yakiwasumbua kutokana na tabia hiyo.
Hiyo ni furaha kwangu kuona kwamba kazi nayofanya inasaidia watu na nguvu zangu hazipotei bure, na ninamshukuru mungu sana kwa hilo. Leo ntaongelea matibabu ya nguvu za kiume kwa watu walioathirika na punyeto ili na wengine ambao hawakupata matibabu yangu wafaidike kama ifuatavyo.

Hakikisha umeacha punyeto kabisa: ili upone tatizo hili hutakiwi kua mtu wa kubadilika mawazo hovyo, kama umeamua kuacha basi acha kabisa na futa kichwani kwako. Jisemee moyoni kwamba mimi Fulani nimeacha tabia hii na sitarudi nyuma. Kama wewe ni mtu wa imani shika kitabu kitakatifu kabisa kulingana na imani yako.

Amsha mfumo wako wa fahamu na mzunguko wa damu sehemu za siri; hii tunaiita booster, kuna virutubisho tunatoa kwa mwezi mmoja ili kushtua nguvu za kiume zilizokua zimepungua kwa kuongeza msukumo wa damu nyingi kwenda sehemu za siri kutokana na madhara haya ya punyeto kisha ataendelea staili ya maisha safi yaani chakula bora na mazoezi na kua sawa kama zamani.. virutubisho hivyo ni vya asili havina kemikali hata kidogo.{unaweza kuwasiliana na mimi kwa namba yangu hapo chini kupata dawa hii  kama unahitaji}.

Mazoezi: kama wewe ni mtu unayeishi bila mazoezi kabisa hutaweza kurudisha nguvu hizo, hivyo unahitaji kufanya mazoezi yeyote angalau nusu saa kwa siku. Inaweza kua kuruka kamba, push ups, kukimbia, kuogelea na kadhalika. Mazoezi haya ndio yanayofanya mzunguko wa damu ue mzuri na wewe usimamishe uume vizuri. Onyo: mazoezi yasiwe makali sana kwani yatakumaliza nguvu za kiume.

Kula chakula bora cha asili; vyakula vya viwandani vina kemikali nyingi sana na ndio vyakula vinaliwa sana kwenye kizazi chetu hichi cha sasa hivi ndio maana shida hizi zamani hazikuwepo ila siku hizi hata kijana mdogo analalamika kuishiwa nguvu za kiume. Kula ugali, maharage, viazi, maziwa mgando, karanga, korosho, mihogo na vyakula vyote vya asili unavyofahamu ila punguza ulaji wa nyama kwani hauna matokeo mazuri kwenye tiba hii.

Kunywa maji mengi sana; kusimama vizuri kwa uume kunategemea sana mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kama mwili una maji mengi ni rahisi damu kwenda vizuri kwenye uume. Nikukumbushe kwamba ni wingi wa damu unaopelekwa sehemu za siri zako na kufanya uume wako usimame vizuri.. pia mwili unatoa kipaumbele vya damu nyingi kwa viungo vinavyotupa uhai kwanza kwa maana nyingine damu yako haiwezi kuacha kwenda kwenye ubongo, figo na moyo kwanza afu iende kwenye uume. Upe mwili sababu za kupeleka damu ya ziada kwenye uume wako kwa kunywa maji mengi.


Tuesday 17 November 2015

KIPINDUPINDU

UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuambukiza wa kuharisha unaosababishwa na vijidudu vya bakteria. Ugonjwa huu hutokana na matumizi ya maji yasiyo safi au chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi. Ugonjwa huu ni wa ghafla na kwa watu wengu hauleti dalili kali sana. Ingawa unatibika, kipindupindu kinaweza kuwa hatari sana na kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Maambukizi Ya Kipindupindu

Kipindupindu hutokana na maambukizi ya vijidudu vya bakteria viitwavyo Vibrio cholera. Vijidudu hivi hukaa kwenye majimaji, na wadudu kama nzi wanaweza kuvihamisha kutoka sehemu moja mpaka nyingine.
Maambukizi hutokea pale ambapo usafi wa maji, chakula, mazingira na binafsi haujazingatiwa. Kwa njia ya chakula vijidudu huingia kwenye utumbo na kisha kushambulia seli za utumbo. Dalili huanza kujionesha masaa 24 mpaka 48 baada ya maambukizi kutokea.

Dalili Za KIpindupindu

Kipindupindu huanza dalili masaa 24 mpaka 48 baada ya maambukizi. Huanza ghafla kwa kuharisha sana bila maumivu yoyote ya tumbo. Mwanzoni choo kinaweza kuwa kizito kidogo lakini baade kuwa chepesi kama maji, muonekano wako hufanana na maji ya mchele (maji baada ya kuosha mchele). Mgonjwa anaweza kuharisha mara nyingi sana kiasi cha kupata choo kwa mfululizo.
Baadae anaweza akaanza kutapika, akapata maumivu ya tumbo,kulegea na mwili kukosa nguvu kutokana na kupoteza maji na madini mengi sana.
Mara nyingi kipindupindu hakiambatani na homa. Wagonjwa wengi hupata dalili ambazo sio kali sana na kupona baada ya matibabu, wengine hupata dalili kali ambazo huchangia upungufu wa maji na mgonjwa kufariki.

Matibabu Ya Kipindupindu

Endapo unahisi una kipindupindu au kuna mtu ana kipindupindu basi wahi au mwahishe hospitali haraka!. Matibabu ya haraka ni muhimu kwa mtu mwenye ugonjwa wa kipindupindu. Kwa kiasi kikubwa ugonjwa hutambulika kwa dalili zake na uchunguzi wa daktari kwa mgonjwa. Pale unapojulikana matibabu ni muhimu ili kuzuia madhara yake. Kwa sababu ugonjwa huu huambukizwa kirahisi kwa njia ya maji na chakula, wagonjwa hutibiwa kwa kuwekwa sehemu za peke yao ili wasiambukize wengine.
Kumuongezea maji ni sehemu  muhimu ya matibabu kutokana na kupoteza maji mengi kwa kuharisha. Maji hupewa kwa njia ya mdomo kama ORS na kwa maji ya dripu.
Dawa kama Tetracycline, Ciprofloxacin na Doxycycline hutumika kwenye kutibu kipindupindu. Hizi zinasaidia kuua vijidudu vya kipindupindu ndani ya mwili.

Kujikinga na Kipindupindu

Usafi binafsi, chakula na mazingira ni muhimu ili kujikinga na kuzuia ugonjwa huu. Husambazwa kwa kutozingatia usafi na hivyo maji au chakula kuingiliwa na vijidudu vya ugonjwa huu. Ili kujikinga na kuzuia ugonjwa huu zingatia yafuatayo;
  • Nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni kila baada ya kwenda chooni
  • Nawa mikono kwa maji safi kabla na baada ya kula chakula au matunda.
  • Osha matunda kwa maji safi kabla ya kula
  • Tumia maji ya kunywa safi yaliyochemshwa au kutakaswa kwa dawa na kuhifadhiwa katika chombo kisafi.
  • Hakikisha unakula chakula ambacho hakijapoa. Kiwe cha moto na kimehifadhiwa katika chombo kisafi.
  • Tunza mazingira yako yawe katika hali ya usafi. Usiruhusu nzi kuruka ruka au kutua kwenye chakula chako.

NINI CHANZO CHA MIAYO?

Kwa kawaida upigaji wa miayo huashiria kuchoka kwa mwili, akili au kujisikia kuchoshwa na jambo au hali fulani. Hali hii hutokea bila kutarajia wala haiepukiki, kama ilivyo kuhema. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kuhusu miayo, binadamu huanza kupiga miayo tangu akiwa tumboni na umri wa wiki 11!
Kuna maelezo mengi tofauti kuhusu suala la kupiga miayo, lakini yanayovutia zaidi ni yale yanayofanywa na mtafiti wa Chuo Kikuu cha Princeton Marekani ambaye amegundua kuwa kitendo cha kupiga miayo huwa kinafanya kazi muhimu sana ya kuupoza ubongo.
Utafiti huo unasheheresha kwa kusema kuwa miayo huwa sawa na ‘reguleta’ ya kurekebisha joto la ubongo, pale joto linapokuwa limezidi kwenye ubongo kutokana na sababu mbalimbali, miayo hutokea kuupoza.
Imeelezwa kuwa watu wengi hupiga miayo wakati wa kipindi cha baridi kuliko kipindi cha joto kwa sababu kipindi cha baridi ubongo huchemka na kitendo cha kupiga miayo huwa kinatokana na mahitaji ya mwili ya kiasili ya kurekebisha hali ya joto kwenye ubongo.
Vile vile utafiti umeonesha kuwa binadamu anapokosa usingizi usiku, joto la ubongo huongezeka kutokana na kufikiri, hivyo anapoamka asubuhi hujikuta analazimika kupiga miayo ili kurekebisha joto lililozidi wakati huo.
Ubongo hufanya kazi kama kompyuta, ambayo hufanyakazi vizuri zaidi inapokuwa imepoa, hivyo maumbile ya kiasili hufanyakazi yake ya kujiendesha yenyewe pale kiungo chochote cha mwili kinapoonekana kuhitaji msaada.
Hata hivyo, utafiti mwingine unaonesha kwamba kupiga miayo kupita kiasi, kunaweza kuwa ni dalili ya tatizo lingine la kiafya, linalosababisha kuongezeka kwa joto kwenye ubongo au kuharibika kwa mfumo wa fahamu.
Kwa upande mwingine, kupiga miayo huwa ni dalili ya mabadiliko ya kimwili, kutoka hali ya uchangamfu kwenda uchovu au usingizi au kinyume chake. Kwa mujibu wa mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Maryland, Marekani, Dk. Robert Provineix, ni sawa pia kusema kuwa utafiti zaidi unahitajika ili kujua nini husababisha binadamu na wanyama wengine kupiga miayo.
Wakati mwingine, upigaji wa miayo mfululizo, huweza kuwa ni dalili ya matatizo ya moyo. Unapokutwa na hali kama hiyo mara kwa mara ni vyema ukaenda kuonana na daktari na kufanyiwa vipimo zaidi. Vile vile upigaji wa miayo mfululizo huweza kuwatokea wagonjwa wa kifafa, muda mfupi kabla ya kushikwa na kuanguka. Hivyo ni vyema kujitambua kama miayo unayopiga ni ya kawaida au siyo. Kwa sababu inawezekana kuwa ni dalili ya tatizo lingine kubwa la kiafya.  
Views: 2480

Thursday 5 November 2015

UTAJUAJE KAMA UNA MIMBA CHANGA?

UTAGUNDUAJE KAMA UNA MIMBA CHANGA?
Mara nyingi ni vigumu mwanamke kugundua kama ameshika mimba siku za mwanzoni hadi pale anapokosa kuona siku zake za hedhi. pamoja na ugumu huo kuna dalili ambazo zinaweza kufanya uhisi kama una mimba katika siku za mwanzoni ambazo ni kuanzia siku ya 18 toka mimba itungwe.
Dalili hizi zinatofautiana kwa kila mtu, wapo ambao wanaweza kuzipata zote na ambao hupata baadhi tu ya dalili hizi na pia wapo ambao hawazipati kabisa.
Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na:
1.JOTO LA MWILI KUPANDA.(basal body temperature stay high)
Wanawake wengi hushindwa kutambua dalili hii pale wanapoipata kutokana na kutokuwa na uelewa
juu ya miili yao.
Hali hii inaonekana katika siku za mwanzo ambambo huweza kudumu kwa muda mrefu kiasi hivyo
kama itadumu zaidi ya siku 18 basi ni vizuri kupima ili kujua kama inatokana na ujauzito au la.
2. KUPATA HAJA NDOGO MARA KWA MARA.(frequent urination)
Kubanwa na haja ndogo mara kwa mara pia inaweza ikawa ni dalili mojawapo ya kuwa na mimba
changa.
3.KUWA MWEPESI KUHISI HARAFU YA VITU MBALI MBALI HASA HARUFU MBAYA.(sensitivity to odors)
Wakati wa mimba changa wanawake wengi wanakuwa wepesi wa kuhisi harufu ya vitu mbali mbali hasa zile harufu zisizo za kupendeza na kumfanya achukie vitu vingi vyenye kutoa harufu hizo.
wakati kama huu si ajabu ukaona mtu hataki mume wake amsogelee kwa kudai anatoa harufu mbaya.
ukiona dalili kama hii inaweza ikawa ni ishara ya kuwa mjamzito hivyo unapaswa kufanya uchunguzi.
4.KUKOSA HEDHI.(missed period)
Kwa kawaida mama mjamzito hapati siku zake za hedhi isipokua anaweza akapatwa na hali ya kuvuja kunakofanana na ile ya hedhi ila damu yake huwa nyepesi sana na hudumu kwa muda mfupi kati ya siku1 au 2 (implantation bleeding) hivyo unapokosa kuona siku zako za hedhi
unapaswa kuchunguza sababu za kukosekana kwa hedhi.
5. KICHEFU CHEFU AU KUTAPIKA.( Nausea or vomiting).
Like   Comment   

Wednesday 4 November 2015

SABABU ZA KUHARISHA KWA WATOTO

SABABU ZA KUHARISHA KWA WATOTO

Utangulizi 

Kuharisha kwa watoto ni tatizo linaloshika nafasi ya pili duniani kwa kusababisha vifo miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano. Inakadiriwa kwamba kwa kila watoto 5 wanaofariki , 1 hufa kwa sababu ya kuharisha. Watoto milioni 1.5 kila mwaka hufa kutokana na kuharisha.
Leo hii, inakadiriwa asilimia 39 tu ya watoto wanaoharisha katika nchi zinazoendelea hupata matibabu sahihi.Hata hivyo, mwenendo wa kitakwimu unaonesha kwamba kumekuwa na mafanikio kidogo tangu mwaka 2000.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwIzhzqtnA1dpbEhnh2xaADC8ae0_cSYeHRbl_ZDjWHm44fzClTOK7aniMRS90pkyAb43WAkyELBZHirPhh-LvKeQWpukTdB03sMVmFBNYSCq0wE9jqPEsCgfpsaFz_tZpnDC1pLO0mqk6/s400/6.jpg
Kuharisha huelezwa kuwa ni upotevu wa maji na madini muhimu kwa mwili wa binadamu (electrolytes) kupitia kinyesi na kupelekea upungufu wa maji mwilini. Katika hali ya kawaida, watoto wachanga hutoa kiasi cha gramu 5 za kinyesi kwa kila kilo ya mtoto (5g/ kg) kwa siku, wakati mtu mzima hutoa wastani wa gramu 200 kwa siku.

Sababu za Kuharisha kwa watoto 

Kuharisha kunaweza kusababishwa na aina mbalimbali za vimelea ingawa pia kunaweza kusitokane na maambukizi ya vimelea (non-infectious causes). Vimelea vinavyosababisha kuharisha ni
Virusi: Virusi vinaongoza katika kusababisha tatizo la kuharisha kwa watoto katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Bakteria: Wanasababisha kuharisha kwa asilimia chache 2-10%. Kuharisha kunakosababishwa na bacteria husababisha upotevu mdogo wa maji ukilinganishwa na virusi. Mfano wa bakteria wanaoweza kusababisha tatizo hili ni Campylobacter, Salmonella, Shigella, na Escherichia coli
Parasite pia husababisha kuhara, lakini aina hii ya kuhara huwa ni sugu zaidi (chronic diarrhea) kwa ujumla na mara nyingi haiambatani na homa, kutapika, na upungufu wa maji mwilini. Giardia lamblia na Cryptosporidium parvum ni moja ya aina hii za parasire wanaosababisha kuhara.

Sababu ambazo hazihusiani na maambukizi ya vimelea yaani noninfectious causes ni pamoja na kula chakula kilichochanganywa na sumu au kumeza sumu, matatizo katika sehemu ya utumbo mwembamba na mnene, na matatizo ya usagaji chakula (metabolic abnormalities).

Kwa vile sababu kuu ya kuharisha ni kutokana na virusi, tutazungumzia aina kuu ya virusi wanaosababisha kuhara. Kuna aina takribani 4 wanaojulikana ambavyo ni Rotavirus, Adenovirus, astrovirus na norovirus. Kati ya hivi jamii ya Rotavirusndio wanaongoza duniani kote katika kueneza na kusababisha kuharisha kwa watoto wachanga na wadogo . Katika nchi zinazoendelea, Rotavirus ndiyo chanzo kikuu cha vifo vinavyotokana na kuhara miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka 5. Rotavirus huathiri wavulana na wasichana kwa uwiano sawa. Hatari zaidi ni kwa wale walio na uzito wa kuzaliwa chini ya gramu 1500 vilevile uzito kati ya gramu 1500-2499. Ukali wa ugonjwa ni mkubwa zaidi kwa watoto wenye umri wa miezi 3-24. Watoto wachanga chini ya miezi 3 wanapata sehemu ya kinga (antibodies) kutoka kwa mama anayenyonyesha na vilevile kinga mtoto aipatayo kupitia kondo la nyuma (placenta) kabla ya kuzaliwa. Kwa maana hiyo basi shambulizi la awali baada ya miezi 3 lina uwezekano wa kusababisha ugonjwa mkali zaidi.

Jamii hii ya Virusi wana uwezo wa kuenea kwa urahisi sana toka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine. Kimsingi wanaenea kwa njia ya kinyesi. Ni rahisi mtoto kupata uambukizi wa rotavirus iwapo atakula chembechembe za kinyesi zenye vimelea hivi. Mtu mwenye vimelea hivi anaweza kuambukiza mtu mwingine hata kabla ya dalili hazijaanza kujionesha kwake au hata siku kadhaa baada ya dalili kujionesha. Mtu aliyeambukizwa anaweza kutoa idadi kubwa ya vimelea hivi kiasi cha virion 1-10 kwa kila mililita ya kinyesi. Ili kuambukizwa kinahitajika kiasi kidogo tu cha hawa vimelea, takribani miligramu 0.000001. Hivyo ni rahisi kuambukizwa kwa kugusana au kwa kushika au kutumia vifaa vyenye maambukizi ya rotavirus. Aidha, rotavirus wamegunduliwa kuwepo katika majimaji ya kwenye kinywa na koo (oropharngeal secretions), ingawa bado haijathibitishwa kama kuna uwezekano wa maambukizi kwa njia ya hewa.

Muonekano wa mgonjwa

Watoto wanaohara kwa sababu ya rotavirusi huwa na dalili kuu tatu ambazo ni homa, kutapika na kuharisha. Kawaida choo kinakuwa cha majimaji sana. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 63 ya watoto wanaolazwa hospitalini kwa tatizo hili wanaonyesha dalili zote 3, asilimia 25 wanakuwa na dalili 2 tu. Wakati mwingine kuharisha kunaweza kujitokeza baadaye baada ya kutapika au homa. Joto la mtoto huwa si kali sana ingawa baadhi ya watoto wanaweza kuwa na joto kali linalozidi nyuzi joto 39 za sentigradi. Kutapika kunaweza kusiwe zaidi ya masaa 24. Vilevile wanaweza kuwa na kuchefuchefu, maumivu ya tumbo (abdominal cramping), kulia pasipo kutulia akibembelezwa (irritability) na uchovu.

Vifo husababishwa na upungufu wa maji mwilini. Upungufu wa maji waweza kuambatana na upungufu na kukosekana uwiano wa madini mwilini (electrolyte imbalance). Aidha kunaweza kusababisha madhara katika figo (ischemic injury to the kidneys) na katika mfumo wa neva (central nervous system) na kusababisha na mtoto kupoteza fahamu (shock).

Inashauriwa kuchunguza kiasi cha maji kilichopotea. Iwapo uzito wa mtoto utakuwa umepungua kwa zaidi ya asilimia 10, mtoto anaweza kuwa na dalili kama
kupoteza fahamu
kuwa na mapigo ya moyo ya kasi
kushindwa kula na kunywa
kuwa na macho yaliyolegea kulegea na kuingia ndani sana (severe sunken eyes)
kushindwa kutoa mkojo kabisa
kutotoa machozi na mdomo kuwa mkavu sana.

Upungufu wa kati ya asilimia 5-10 ya maji mwilini, husababisha
macho ya mtoto huingia ndani (sunken eyes)
ngozi kurudi taratibu pindi inapovutwa (loss of skin turgor)
mapigo ya moyo kuwa kasi
kuwa na ubonyeo katika sehemu ya mbele ya kichwa (depressed anterior frontanele)
uchovu
kiu na kunywa maji kwa haraka
mtoto kutoa machozi kidogo sana pindi anapolia
midomo kuwa mikavu na
kupumua kwa haraka kuliko kawaida

Chini ya asilimia 5 mtoto huwa na
kiu
ngozi inayorudi taratibu pindi ikivutwa
macho yanaweza kuingia ndani na
uchovu.

Unapoona dalili hizi wakati mtoto wako anaharisha unapaswa kumpeleka haraka kituo cha afya ili kupata ushauri wa wataalamu wa afya.

Uchunguzi 

Kipimo cha choo: hujumuisha pia uchunguzi wa vimelea.
Kipimo cha antigeni cha Rotavirusi (Rotavirus antigen tests) ingawa asilimia 50 ya majibu yanaweza kuwa si sahihi (false-negative) hasa pale panapokuwa na damu kwenye choo.
Kupima kiwango cha sukari mwilini (blood glucose level)
Chembechembe nyeupe za damu kutambua maambukizi ya bakteria.
Kupimo cha figo (Renal function Test and electrolytes)
Vipimo vingine kutegemea na hali ya mgonjwa.

Matibabu 
Ingawa yawezekana mtoto kupona bila hata matibabu lakini ni jambo muhimu kuchunguza madhara yanayoweza kusababishwa na upungufu wa maji mwilini. Ieleweke kuwa watoto wapo katika hatari kubwa zaidi ya ya kupungukiwa na maji mwilini kutokana na kuharisha, hivyo basi msingi wa matibabu ni kurudisha kiasi cha maji kilichopotea.

Hali kadhalika, matumizi ya madini ya zinc yamehusishwa na kupungua kwa makali ya ugonjwa na kupunguza muda wa kuharisha.

ORS ambayo ni mchanganyiko wenye uwiano mzuri wa chumvi na sukari ni aina ya tiba inayopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya matibabu. Uwiano uliopo katika ORS huwezesha utumbo wa mtoto kufyonza vizuri maji na madini mengine.

Matibabu ya kuharisha kwa watoto yanaweza kugawanywa katika awamu kuu mbili:
Kurudisha maji yaliyopotea (rehydration)
Kuendelea kuupa mwili maji kwa ajili ya mahitaji ya kila siku (Maintenance)

Mlezi hushauriwa namna ya kutengeneza mchanganyiko huu ORS kulingana na hali ya mtoto. Kwa mama wanaonyonyesha, wanashauriwa kuendelea kumnyonyesha mtoto mgonjwa huku akimpa mlo wa kawaida wa kila siku. Ikiwezekana, ni vema pia kuendelea kumpa mtoto maji ya ziada. Kama mtoto akitapika, mzazi/mlezi anashauriwa kusubiri kwa angalau dakika 5-10 kabla ya kuendelea tena kumnywesha kidogo kidogo (kwa mfano, kijiko kila baada ya dakika 2-3).

Watoto walio na hali mbaya na wale waliopoteza zaidi ya asilimia 10 hawana budi kupewa maji kwa njia ya mishipa ya damu yaani intravenous fluids.

Kwa vile chanzo kikuu cha kuhara kwa watoto ni maambukizi ya virusi, haishauriwi kutumia antibiotics kama sehemu ya matibabu. Hata hivyo antibiotics zinaweza kutumika tu pale ambapo itathibitika kuwa kuharisha kumesababishwa na bakteria.

Dawa za kuzuia kuharisha kama vile Loperamide hazishauriwi kwavile athari zake ni mbaya zaidi kwa mtoto kuliko faida.

Namna ya kuzuia maambukizi 
Kuzingatia usafi wa chakula (kupika na kuhifadhi).
Kunawa mikono kila baada ya kutoka chooni, kabla ya kushika chakula na wakati wa kula
Kuwa makini na watoto wanaoharisha ikiwezekana kuwatenga na wenzao
Matumizi ya Chanjo: Usalama wa chanjo ya Rotavirus bado haujathibitishwa rasmi hasa kwa watoto chini ya wiki 6. Aidha chanjo hii imekuwa ikihusishwa na kutokea kwa matatizo katika utumbo mkubwa na mdogo.

KARIBUNI UONGEE NA KIWALE BRASTO

LISHE KWA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

LISHE KWA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


Na Dk. Fadhil Emily

BRASTO KIWALE:

 Anapenda kukupa maelezo kuhusiana na lishe ambayo inaweza kusaidia kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Imesekekana kuwa baadhi ya vyakula vikitumika mara kwa mara vyaweza kupunguza na kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na maumivu. Tumejaribu kuelezea baadhi ya vyakula ambavyo tunaamini kuwa vikitumika vinaweza kuondoa tatizo hilo, navyo ni:-


1. Mdarasini + Asali (Sermon + Honey)
Hiyo imedhibitishwa na watalaamu kuwa unweza kutibu upungufu wa nguvu wa kiume. Unapotumia mdarasini pamoja na asali mara kwa mara unaongeza nguvu za kiume na kuondoa maumivu unayoyapata.
2. Maua ya Yerusalem (Star of Jerusalem)
Ikiwa mtu mwenye upungufu wa nguvu za kiume atakuwa akitafuna vikonye vitatu vya maua meupe ya Yerusalem. Acaroids Acid ina virutubisho muhimu ambapo watu wa biolojia  wameamini kuwa kiwango kikubwa kinauwezo wa kuratibu swala hilo la nguvu za kiume
3. Karanga mbichi zisizokobolewa
Watu wa biolojia (Biologist) wanasema karanga zisizokobolewa zina protini (protein) muhimu ambayo inamchanganyiko wa Carolis ambayo kwa hakika imethibitishwa kuwa, nayo ni msaada mkubwa kwa upungufu wa nguvu za kiume.Matatizo ya nguvu za uzazi ikiwa ni pamoja na upungufu wa nguvu za kiume na homoni (hormone) za kike, kitalaamu ni kasoro ambazo husababishwa na vijidudu na bacteria ambazo kwa hakika ukitaka kupata uponyaji, yakupasa utumie viinirishe au virutubisho vinavyotoka katika vyakula mbalimbali ambavyo hakika vyaweza kuratibu mfumo wa homoni (hormone) moja kwa moja na si kutumia sindano na vidonge ambavyo havikusaidii kurudisha virutubisho kwani vyatumika kama kupunguza au kupooza kuondoa maumivu tu (Pain Killer).

“Pain Killer” ikishaisha mwili mwako, hali ya zamani ya upungufu wa nguvu za kiume na maumivu hurudi tena na tatizo linabaki pale pale.

Inasemekana kuwa kwa asilimia nyingi vyakula vichache vilivyotajwa hapo juu vikitumika sawasawa na mara kwa mara huweza kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

 hali ya tatizo na sio kuponya ila ukitumia hivyo vyakula tulivyoeleza hapo juu unaweza kuponywa nahuo ugonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume na maumivu.

Kwa maelezo zaidi fika katika ofisi za
Fathaget Sanitarium Clinic Mbezi Beachi Tangi Bovu
Kutana na Dk. Fadhil Emily
Simu: 0758278349
Blogu: kiwale1990.blogspot.com