Saturday 2 January 2016

Maana ya mkabala, Maana ya mkabala wa ki-marx, U- Marx

B. F. KIWALE
P.O BOX 774
IRINGA


© Kiwale, F. Brasto 2015


ISBN 9976 911 49 1




chapa ya kwanza 2015, December. 28.

Haki zote zimehifadhiwa. hakuna sehemu ya kazi hii itakayo ruhusiwa kuirudia kuitengeneza, kwa namna yoyote ile, bila ruhusa ya mwandishi au B. F  Consult P.O. Box 774, IRINGA.




Printing and publishing consultancy by
KAD Associates/ TFC, P.O Box 32746,


Dar es Salaam, Tanzania.
                                                                














1.0.  Utangulizi
1.1. Maana ya mkabala
Mkabala ni utaratibu ,mtazamo au kanuni katika kuhakiki kazi za fasihi. Mitazamo ya wahakiki wa kazi ya fasihi hutofautiana baina ya mhakiki mmoja na mhakiki mwingine.
1.2. Maana ya mkabala wa ki-marx
Mkabala wa ki-marx ni mkabala ambao misingi yake mikuu ni mawazo yaliyoasesiwa na Karlmax na Fredrich Angels (1818-1895), mkabala huu umejikita katika nyanja mbalimbali ambazo ni uchumi, historia, jamii na mapinduzi, mawazo yamkabala wa ki-marx hayaegemei katika dhana dhahania bali ni katika uhalisia au uyakinifu.
2.0.  Mawazo haya ya ki-marx yamejidhihirisha katika kitabu cha Vuta n’kuvute kilichoandikwa na Shafi Adam Shafi (1999), na kitabu cha “Mwalimu Mkuu Wa Watu” kilichoandikwa na Paschally B.Mayega(2006).
2.1  Kwa kuanza na kitabu cha “Vuta n,kuvute” yafuatayo ni mawazo makuu ya u-marx yalivyojidhihirisha katika kitabu hiki.
Katika historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi zake, namna yake ya kufikiri, mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji mali yaani, jinsi uchumi, uzalishaji, mgawanyo na umilikaji wa mali  unavyoendeshwa. Wazo hili la u-marx linajidhihirisha katika kitabu hiki cha “Vuta n’kuvute,” pale ambapo watu wa Unguja na Pemba walipoanzisha harakati za kujikomboa kiuchumi kutoka katika minyororo ya kunyonywa na wakoloni wa kiingereza. Uchumi wa Zanzibar ulikuwa mikononi mwa wazungu ambao walikuwa wanamiliki njia zote za uzalishaji mali, wakati waafrika hawakumiliki chochote. Kutokana na hali hii, Denge na kundi lake wakaamua kuanzisha harakati katika kuwakomboa waafrika
kiuchumi kwa kuchukua njia kuu za uzalishaji mali kutoka kwa wazungu wachache na kuziweka mikononi mwa waafrika walio wengi.
Katika historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi zake, namna yake ya kufikiri, mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya  mfumo wa uzalishaji mali, yaani jinsi uchumi, uzalishaji, mgawanyo na umilikaji wa mali unavyoendeshwa. Wazo hili la u-marx limejidhihirisha katika kitabu cha “Mwalimu Mkuu wa Watu” kana kwamba mfumo wa uzalishaji mali  pamoja na umilikaji wa mali unavyoendeshwa katika hali ambayo haikuwapa wananchi fursa ya kushiriki katika maendeleo ya nchi yao jambo lililompelekea
mwalimu pamoja na wananchi wengine kuanzisha harakati za kuondoa utawala uliopo. Katika ukurasa wa 8 msanii anasema;
                        “wananchi walipangwa zefe na
                           maandamano yalianza taratibu,
                            shwari bila vurugu zozote”.
Maandamano hayo yalitokana na kasoro zilizopo katika mfumo mzima wa uzalishaji mali ulivyoendeshwa katika jamii ile.
Pia katika kitabu cha “morani” kilichoandikwa na E. Mbogo mwaka 1993 wazo hili la u-marx  limejidhihirisha pale ambapo  namna ya kufikiri kwa wahusika Jalia, Dongo na wenzake kulichangiwa na jinsi mfumo wa uzalishaji mali ulivyokuwa unaendeshwa. Mfumo huo ulikuwa umejaa ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi  ndio maana Jalia, Dongo na wenzake wakaanzisha harakati za mapinduzi. Katika  ukurasa wa 41 mwandishi anasema 
                   “Morani waungane na umma. Waungane kuiendeleza kutafuta nguzo ya uswezi”   
Historia ya mwanadamu huakisi harakati zinazoendelea katika matabaka ya kiuchumi, jamii au uzalishaji  yanayoathiri mabadiliko ya muundo wa matabaka na hivyo  kujitokeza katika tabaka tawala na tawaliwa  ambavyo huwamo katika mapambano na katika harakati za kugombea uchumi, siasa na faida za jamii.wazo hili la u-marx linajitokeza katika kitabu hiki pale ambapo kulikuwa na matabaka kati ya wazungu, wahindi na waafrika kutokana na matabaka haya kulikuwa na ubaguzi, ilikuwa si rahisi kwa mzungu kuchanganyikana na mwafrika na vilevile ilikuwa si rahisi kwa mhindi kuchanganyikana  na mwafrika. Kwa upande wa makazi, waafrika waliishi ndani ya vibanda vidogo vidogo vya uswahilini, wakati wazungu na wahindi waliishi kwenye marosheni na majumba ya watukufu. vilevile kwenye huduma nyingine waafrika walikwenda kwenye maduka ya mchangani na darajani ambayo yaliuza bidhaa hafifu, wakati wazungu na wahindi waliingia ndani ya maduka ya shangani na baghani ambayo yaliuza vitu kwa bei ya ghali na yalitoa huduma bora za kila namna. Kwa upande wa sehemu za starehe  waafrica walistarehe sehemu iitwayo Raha leo, wazungu walistarehe katika English club na wahindi walistarehe katika Karimjee club. Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo ya matabaka, Denge pamoja na kundi lake wakaamua kuanzisha harakati za kutokomeza utawala huo wa kiingereza  kwa kutawanya vitabu vyenye mawazo ya ki-marx.
Historia ya mwanadamu huakisi harakati zinazoendelea katika matabaka ya uchumi, jamii au uzalishaji mali yanayoathiri mabadiliko ya muundo wa matabaka na hivyo kujitokeza katika tabaka tawala na tawaliwa ambavyo huwamo katika mapambano na katika harakati za kugombea uchumi, siasa na faida za jamii . wazo hili la u-marx limejidhihirisha katika kitabu cha “Mwalimu Mkuu wa Watu” pale msanii anapoonesha matabaka katika jamii ile ambapo kuna tabaka tawala lililoongozwa na mawaziri wa serikali pamoja na raisi, na tabaka la chini likiongozwa na mwalimu mkuu na wananchi wengine wa tabaka la chini. Hivyo harakati zilizofanywa na mwalimu mkuu zilikuwa na lengo la kugombea uchumi, siasa pamoja na faida za kijamii. Katika ukurasa wa 43-44 msanii anaonesha harakati zilizofanywa na mwalimu  mkuu pindi alipokuwa ameshitakiwa na Fredrick de witts, mwalimu mkuu aliandika ujumbe kwa wananchi akisema;
“Salamu enyi ndugu wapendwa Mungu ni mwema. Akikupa chakula kigumu, hukupa pia na meno magumu.Nawatumieni msaidizi atakayewatia faraja na kuwaelekeza yote ambayo ningewaelekeza. Msikilizeni na mfuate maelekezo yake nanyi hamtakuwa yatima tena: eleweni kuwa njia ya ushindi ni ngumu, lakini jipeni moyo kwa maana siku ya ushindi iko karibu. Usiku mzito ni pale karibu na kucha. Ni mimi ndugu yenu Ngowe Boniface.
Vilevile katika kitabu cha “Morani” kimeelezea suala ya matabaka mfano tabaka la juu la wenye pesa ambalo ndilo linalomiliki njia kuu za uzalishaji mali liliwahusisha mhusika Nungunungu na Mlemeta, na tabaka la chini ambalo lilikuwa likinyanyaswa na tabaka la juu kupitia vyombo vya dola likiwahusisha wahusika kama Jalia, Dongo na wenzake. Hivyo ikawapelekea wahusika hao wa tabaka la chini kuanzisha harakati dhidi ya kupambana na tabaka tawala ili kuleta ukombozi katika tabaka la chini ili kugombea uchumi, siasa na faida za jamii. Katika uk. 66, mwandishi anaonesha jinsi vyombo vya sheria vinavyowatendea watu wa tabaka la chini  kutokana na kutokuwa na sauti       yoyote katika jamii.
Ulazini wa binadamu umeundwa na itikadi, thamani ya kitu na namna ya kufikiri na kuhisi ni kupitia hivi, mwanadamu huona ulimwengu wake nay ale anayoyaona  na hayo yanayomzunguka kuwa ni ukweli. Wazo hili la u-marx linajitokeza katika kitabu hiki, kwa kitendo cha Denge na kundi lake kugundua kuwa wananyonywa, wanaonewa na kugandamizwa na wakoloni ulikuwa ni ukombozi wa kifikra ndio maana walianzisha harakati za kudai haki zao za msingi. Pia kitendo cha Yasmini kuona kuwa baadhi ya mila na desturi zinamnyanyasa mwanamke na kuamua kuachana nazo inadhihirisha wazi kuwa Yasmini alikuwa na uwezo wa kufikiri na kuona mbali.
Ulazini wa binadamu umeundwa na itikadi, thamani ya kitu na namna ya kufikiri na kuhisi ni kupitia hivi, mwanadamu huona ulimwengu wake nay ale anayoyaona na hayo yanayomzunguka kuwa ukweli. Wazo hili la u-marx limejidhihirisha katika kitabu hiki cha “Mwalimu Mkuu wa Watu” kwa kuwa msanii anamchora mwalimu mkuu kwa jinsi ambavyo namna yake ya kufikiri, kuhisi pamoja na utashi wa hali ya juu ndio uliomfanya kuona uovu uliokuwa ukitendeka katika tabaka tawala. Uovu huo ni pamoja na serikali kuruhusu wawekezaji uchwara ambao hawakuwa na tija yoyote kwa wananchi walio wengi pamoja na rushwa iliokithiri miongoni mwa viongozi wakubwa wa nchi, na ndicho kitu kilichompelekea mwalimu mkuu kuanzisha harakati dhidi ya tabaka tawala.
Pia katika kitabu cha “kilio chetu” kilichoandikwa na Medical Aid Foundation, wazo hili la u-marx  limejidhihirisha pale ambapo msanii amemtumia mhusika mjomba , ambaye aliona kuwa ni muhimu kuwapa watoto elimu ya kijinsia, lakini jamii iliona kuwa kuwapa watoto elimu ya kijinsia ni kuwafundisha watoto kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo kitu ambacho si sahii.
Ubepari kama njia ya uzalishaji mali unatabiriwa na kuvunjiliwa mbali kutokana na juhudi za wafanyakazi au utaishia wenyewe kutokana na mbegu za maangamizo zilizosheheni. Wazo hili la u-marx linajidhihirisha katika kitabu hiki cha “Vuta n’kuvute” pale ambapo harakati za Denge na kundi lake kutawanya vitabu na magazeti yaliyokuwa yakipinga siasa ya ukoloni wa kiingereza. Pia Denge alisomeshwa na waingereza na huyo ndiye aliyekuja  kupinga utawala wa kiingereza ambapo alipata elimu na hiyo elimu ilimsaidia ndio maana akaanzisha harakati za kupinga serikali ya kikoloni.
Ubepari kama njia ya uzalishaji mali unatabiliwa na kuvunjiliwa mbali kutokana na juhudi za wafanyakazi au utaishia wenyewe kutokana na mbegu za maangamizo zilizosheheni. Wazo hili la ki-marx linajidhihirisha katika kitabu cha “Mwalimu Mkuu wa Watu” kwani mwandishi anaonesha mbegu za maangamizo zilizopandwa na serikali kwa kuwapa elimu mwalimu mkuu wanajeshi pamoja na wanafunzi ambapo kutikana na uovu uliofanywa na serikali ulimfanya mwalimu mkuu pamoja na wananchi kuwa na upeo wa kuyaona maovu hayo na hivyo kuanzisha harakati dhidi ya uovu huo.
Wazo hili la umarx pia limejidhihirisha katika kitabu cha  “ kivuli kinaishi” kilichoandikwa na Said A. Mohamed, pale ambapo ubepari  uliokuwepo dhidio ya serikali ya Bi kirembwe ndio uliopelekea  kuvunjiliwa mbali kwa utawala wake kupitia wahusika Mtolewa wali na wengineo ambao walikuwa wafanyakazi wa tabaka la chini ambao walikuwa wakigandamizwa katika nyanja zote za kimaisha mfano kichumi kisiasa na kijamii. Katika uk. wa 70 msanii anasema;
               “Hamtaweza kufahamu mpaka niwatoeni  mzigo mlionao …
                hamtatambua mpaka nikufumbueni macho na kukuzibueni masikio…”                                        
Mtolewa aliwafumbua macho wali wenzake kwa kuwalisha unga wa rutuba elimu inayomfanya mtu ajitambue na atambue nafasi yake katika jamii na aweze na kuwaelimisha wenzake.   
Njia za kusaidia na labda hata kuharakisha kuangamizwa kwa ubepari ni kudadisi, kukosoa, kushutumu, kulaumu na kufichua ukatili uliopo katika itikadi ya kibwenyenye inayouimarisha ubepari. Wazo hili la u-marx linajidhihirisha katika kitabu hiki pale ambapo Denge na kundi lake walipoandaa vipeperushi na maandamano ya kushutumu, kudadisi, kukosoa, kulaumu na kufichua ukatili uliopo katika serikari ya kikoloni. Denge alikuwa mwanaharakati wa kupinga utawala wa mwingereza visiwani Unguja na Pemba  na katika harakati zake alisambaza vitabu vya Karlmarx, magazeti yanayopinga ukoloni pamoja na makaratasi ya uchochezi dhidi ya makoloni hayo.
Njia za kusaidia na labda hata kuharakisha kuangamizwa kwa ubepari ni kudadisi, kukosoa, kushutumu, kulaumu na kufichua ukatili uliopo  katika itikadi ya kibwenyenye inayouimarisha ubepari. Wazo hili limethibitishwa katika kitabu hiki cha “Mwalimu Mkuu wa Watu” kwani msanii amemchora mwalimu mkuu kwa jinsi ambavyo alikosoa, alilaumu na kufichua ubatili uliofanywa katika serikali hiyo, ubatili huo ni pamoja na kuruhusu wawekezaji wasio na tija katika nchi, vilevile rushwa iliyokithiri miongoni mwa viongozi wakubwa wa nchi.
Pia katika kitabu cha Kivuli kinaishi wazo hili la u-marx limejitokeza pale ambapo mwandishi amemtumia mhusika Mtolewa  alipowalisha wari unga wa rutuba  kwa lengo la kukosoa, kushutumu, kulaumu na kufichua ubatili uliokuwepo katika serikali ya Bi kirembwe katika jamii ya Giningi.
 Nadharia ya ki-marx inahusishwa na kuandamana pamoja na hata kuelezeka kwa matendo  ya utekelezaji dhidi ya mfumo mzima wa kibepari. Wazo hili la ki-marx linajidhihirisha katika kitabu hiki pale ambapo Denge na kundi lake walipoamua kuanzisha maandamano makubwa na Denge alikuwa mstari wa mbele akiwa na makaratasi aliyokuwa anayagawa kwa mtu yoyote aliyemkaribia. Makaratasi hayo yalikuwa yanapinga ukoloni ambao ulikuwa unawanyonya na kuwagandamiza watu wa tabaka la chini.
Nadharia ya ki-marx inahusishwa na kuandamana pamoja na hata kuelezeka kwa matendo ya utekelezaji dhidi ya mfumo mzima wa kibepari. Wazo hili la u-marx limejitokeza katika kitabu hiki, pale ambapo mwalimu mkuu aliongoza maandamano pamoja nawananchi wengine dhidi ya uovu uliotendwa na viongozi wa serikali.mfano katika ukurasa wa 8 msanii anasema;
 “ maandamano hayo yalijumuisha watoto, vijana, wazee, akina mama na hata vilema na ulemavu          wao. Waliendelea mbele na kukata kushoto kuingia katika barabara iendayo mojo kwa moja kiwandani.”

Katika kitabu cha Morani wazo hili la u-marx limejidhihirisha pale ambapo mtunzi amewatumia  wahusika Jalia, Dongo na wenzake walivyokuwa mstari wa mbele katika  kupiga vita uhujumu uchumi, kuandaa maandamano yaliyolenga kupambana na mfumo mzima wa serikani iliopo madarakani  uliokuwa umejaa rushwa, uhujumu uchumi na uongozi mbaya. Katika uk.41 msanii anasema;
                “Morani waungane na umma kuiendeleza kutafuta nguzo ya uswezi”









Dhana ya Lugha, Sifa za lugha, Tabia za lugha, Matumizi na umuhimu wa lugha

B. F. KIWALE
P.O BOX 774
IRINGA


© Kiwale, F. Brasto 2015


ISBN 9976 911 49 1




chapa ya kwanza 2015, December. 28.

Haki zote zimehifadhiwa. hakuna sehemu ya kazi hii itakayo ruhusiwa kuirudia kuitengeneza, kwa namna yoyote ile, bila ruhusa ya mwandishi au B. F  Consult P.O. Box 774, IRINGA.




Printing and publishing consultancy by
KAD Associates/ TFC, P.O Box 32746,
Dar es Salaam, Tanzania.













1.0  Utangulizi
1.1. Dhana ya Lugha.
Wataalamu mbalimbali wametoa ufafanuzi kuhusu dhana ya Lugha kama ifuatavyo.

Trudgil, (1974) anasema “Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake.”

Sapir, (1921) anasema “Lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie  kuwasilishia mawazo,  maoni na mahitaji” mfumo huu hutumia ishara ambazo  hutolewa kwa hiari.

Weber, (1985) anasema  “Lugha ni mfumo wa mawasiliano ya mwanadamu ambao hutumia mpangilio  maalumu wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi  kwa mfano mfano mofimu, maneno na sentensi” pia anadai kuwa lugha ni mfumo wowote wa mawasiliano ya  watu kwa mfano lugha ya kifaransa na lugha ya kihindi.

TUKI, (1990) masema “Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana.”

Todd,  (1987) anadai kuwa” lugha ni mfumo wa ishara za sauti ambazo kwazo watu huwasiliana.”

Barber, (1979) anaeleza kuwa “Lugha ni utaratibu wa kupeana habari unaotumia alama za sauti na  unaotumiwa na kundi fulani la watu kwa nia ya kuwasiliana na kushirikiana katika jamii.”

Cook (1969)  naye anasema” lugha ni mfumo wa sauti na ishara za kisarufi zinazotumika kuwasiliana na kupokezana utamaduni.”

Wataalamu hawa wote wanaelekea kukubaliana kuwa Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano baina yao.

Kwa ujumla Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa na watu wenye utamaduni unafanana ili kuwasiliana.

1.2.  Sifa za lugha
Lugha ina sifa zake kama zifuatazo; Lugha lazima imuhusu mwanadamu, lazima iwe na sauti ambazo hutamkwa kutoka kinywaji mwa mwanadamu, lugha hufuata mpangilio wa vipashio unaoleta maana, lugha ina sifa ya kujizalisha na pia lugha ina sifa ya kusharabu.

1.3.  Tabia za lugha
Pia lugha ina tabia zake kama zifuatazo; Lugha ina tabia ya kukua kutokana na jinsi inavyoendelea  kutumiwa na jamii, Lugha ina tabia ya  kuathiri na kukubali kuathiriwa kutokana na mwingiliano wa Lugha.

1.4.  Matumizi na umuhimu wa lugha
Lugha ina matumizi na umuhimu wake katika jamii kama vile, kutumika kuwasiliana, kuunganisha jamii, kujenga jamii, ni  chombo kinachoweza kuliifadhi na kueneza amali za jamii pia lugha  ni utambulisho wa jamii fulani.

1.5.  Dhana ya utambulisho
Utambulisho ni ubainisho unaomdhihirisha mzungumzaji Fulani kuwa yuko tofauti na  mzungumzaji mwingine au jamii Fulani iko tofauti na nyingine.

Utambulisho wa  mzungumzaji ni upekee alionao mzungumzaji katika kutumia Lugha yake utambulisho wa jamii ni ule upekee wa jamii.  Anaobainishwa kwa misingi ya kiutamaduni ambayo iko tofauti na misingi ya tamaduni  za jamii nyingine.

Utambulisho wa mzungumzaji huweza kubainishwa, kwa kutumia vibainishi vya kijamii na kiisimu. Vibainishi vya kijamii ni vibainishi ambavyo hufungamana na utamaduni wa jamii ya mzungumzaji na vibainishi vya kiisimu ni vibainishi vinavyohusu Lugha ya mzungumzaji

1.6.  Vibainishi vya kiisimu
Vifuatavyo ni vibainishi vya kiisimu vinavyothibitisha utambulisho halisi wa  mzungumzaji unaokubalika na yeye  mwenyewe pamoja na jamii yake. vibainishi hivyo ni  kama vile mkazo, lafudhi, kiimbo, lahaja, matamshi  ya sauti, maneno na hata miundo ya lugha
Mkazo, ni kipengele cha kiisimu kinachohitajia unguvunguvu wakati wa utamkaji mkazo ni kibainisho cha kiisimu ambacho kinaweza kumtambulisha mzungumzaji.  Mfano; Katika Kiswahili mkazo unatokea katika silabi ya pili kutoka mwisho mwa neno mfano katika neno “mama mdogo   mkazo upo kwenye silabi ya pili kutoka mwishoni .  Pia katika maneno ya kiingereza mkazo hutokea katika silabi ya mwanzoni mwa neno. Mfano neno “Baby sit katika neno hili  unguvunguvu umetokea katika silabi ya kwanza,   hivyo mkazo ni kibainisho cha kiisimu kinachoweza  kumtambulisha mzungumzaji.

Lahaja  ni vilugha vidogo vidogo vya Lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia lahaja za lugha moja zatofautiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati Mfano: Lugha za Kiswahili hutofautishwa kulingana na maeneo yake kama; kiamu (Kisiwani kwa lamu), kimvita (mjini mombasa), kiunguja (kisiwani Zanzibar). Pia hata lugha ya kiingereza ina lahaja mbalimbali na lahaja zake zinavyozungumzwa ni tofauti mfano; uingereza, marekani, uhindi, Australia na maeneo mengine./

Kiimbo ni hali ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti mtu anapozungumza. kiimbo husaidia kuleta maana kamili ya sentensi iliyokusudiwa. Mfano kama ni swali  mshangao au maelezo.

Mfano:  Dada amekuja? (swali)
              Dada amekuja. (Maelezo)
              Dada amekuja!  (mshangao)

Lafudhi ni namna ya uongeaji wa kitarafa au ni namna ya mtu ya kuyatamka maneno ambayo humtambulisha mahali anakotokea mfano, mtu wa Arusha huwa na lafudhi tofauti na mtu wa Makete.

Matamshi ya sauti, matamshi ndio humbainisha msemaji kuwa lugha yake ya kwanza ni ipi.
Mfano wapare wameathirika sana na lugha mama hivyo hushindwa kutofautisha kati ya “s” na “th” husema “thatha” badala ya “sasa.” Pia wanyakyusa  hushindwa kutofautisha kati ya “v” na “f” husema “fiatu fyangu”  badala ya “viatu vyangu” Hivyo matamshi ya sauti huweza kumtambulisha mzungumzaji.

Miundo ya lugha, mzungumzajji huweza kutambulishwa kwa miundo ya lugha, kwa mfano katika lugha ya kinyamwezi na kimatendo kama  wanaongea na mtu wanayemheshimu wanatumia uwingi badala ya umoja hata kama mtu anayeongea naye yupo mmoja tu.
Mfano:  “Mtafika saa ngapi?” badala ya  “Utafika saa ngapi?”

1.7.  Vibainishi vya kijamii
Baadhi ya vibainishi vya kijamii vinavyothibitisha utambulisho halisi wa mzungumzaji unaokubalika na yeye mwenyewe pamoja na jamii yake ni mavazi, chakula, utamaduni, mila na desturi, lugha, historia ya jamii imani

Chakula hiki ni kibainishi cha kijamii kinachothibitisha utambulisho halisi wa mzungumzaji kwa mfano: “Ndizi” ni chakula kinachopendwa sana na wanyakyusa  wachaga na wahaya, vilevile  viazi mviringo ni chakula kinachopendwa sana na  wakinga. Hivyo chakula huweza kumbainisha mzungumzaji.

Lugha, huweza kuutambulisha mzungumzaji kuwa ni wa jamii gani, mfano ukimwona mtu anazungumza lugha ya kikinga basi unajua kuwa huyu ni mtu wa makate au ukimwona mtu anazungumza kihaya unajua kuwa huyo ni mtu wa Bukoba, vilevile ukimwona mtu anazungumza kimasai basi utajua kuwa huyo mtu ni mmasai.

Mavazi, haya pia ni kibainisho halisi cha mzungumzaji, mfano; vazi la kimasai, kama mtu amevaa vazi la kimasai ukimwona utamtambua kwa vazi lake kuwa huyu ni mmasai, pia hata ukimwona mtu kavaa buibui utajua kuwa huyu ni muislamu, au ukimwona mtu kava vazi la kinaijeria utajua kuwa huyu ni mnaijeria. Hivyo mavazi nayo ni kibainisho cha kinachoweza kumbainisha mzungumzaji.

Mila na desturi, ni utaratibu na kanuni katika jamii fulani. Katika jamii zetu kila jamii ina utaratibu na katuni zake katika mfumo mzima wa maisha. Mfano. Kabila la wakinga wana utaratibu wao, mfano, mdogo anapomsalimia mtu mkubwa lazima apige magoti wakati baadhi ya jamii zingine hazina huo utaratibu. Hivyo basi ukiwaona watu wanasalimiana huku wakipiga magoti utawatambua kuwa watu hawa ni wa jamii fulani kulingana na mila na desturi zao.


2.0.  Hitimisho.
Hivyo vibainishi vya kiisimu na vibainishi vya kijamii huthibitisha utambulisho halisi wa mzungumzaji unaokubalika na yeye mwenyewe pamoja na jamii yake kwa ujumla.











 3.0.  MAREJEO.
Besha,  R.  (1994), Utangulizi wa lugha na isimu, Dar  es salaam University Press.
Habwe, J.  na  Karanje, P. (2004), Misingi ya sarufi ya kiwahili Nairobi Phonix Publishers.
Massamba, D. na wenzake (2004), Fonolojia ya Kiswahili sanifu (fokisa)  sekondari na vyuo TUKI

















Friday 1 January 2016




NIPENDE KUWATAKIA MWAKA MPYA MWEMA
  ILA    ANZA PAMOJA NA BWANA



NAWATAKIA MWAKA MPYA MWEMA KWENU