B. F. KIWALE
P.O BOX 774
IRINGA
© Kiwale, F. Brasto 2015
ISBN 9976 911 49 1
chapa ya kwanza 2015, December. 28.
Haki zote zimehifadhiwa. hakuna sehemu ya kazi hii itakayo ruhusiwa kuirudia kuitengeneza, kwa namna yoyote ile, bila ruhusa ya mwandishi au B. F Consult P.O. Box 774, IRINGA.
Printing and publishing consultancy by
KAD Associates/ TFC, P.O Box 32746,
Dar es Salaam, Tanzania.
1.0. Utangulizi
1.1. Maana ya mkabala
Mkabala
ni utaratibu ,mtazamo au kanuni katika kuhakiki kazi za fasihi. Mitazamo ya
wahakiki wa kazi ya fasihi hutofautiana baina ya mhakiki mmoja na mhakiki
mwingine.
1.2. Maana ya mkabala wa ki-marx
Mkabala
wa ki-marx ni mkabala ambao misingi yake mikuu ni mawazo yaliyoasesiwa na
Karlmax na Fredrich Angels (1818-1895), mkabala huu umejikita katika nyanja
mbalimbali ambazo ni uchumi, historia, jamii na mapinduzi, mawazo yamkabala wa
ki-marx hayaegemei katika dhana dhahania bali ni katika uhalisia au uyakinifu.
2.0. Mawazo haya ya ki-marx yamejidhihirisha
katika kitabu cha Vuta n’kuvute kilichoandikwa na Shafi Adam Shafi (1999), na
kitabu cha “Mwalimu Mkuu Wa Watu”
kilichoandikwa na Paschally B.Mayega(2006).
2.1 Kwa kuanza na kitabu cha “Vuta n,kuvute” yafuatayo ni mawazo makuu
ya u-marx yalivyojidhihirisha katika kitabu hiki.
Katika
historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi zake, namna yake ya
kufikiri, mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji mali
yaani, jinsi uchumi, uzalishaji, mgawanyo na umilikaji wa mali unavyoendeshwa. Wazo hili la u-marx
linajidhihirisha katika kitabu hiki cha “Vuta
n’kuvute,” pale ambapo watu wa Unguja na Pemba walipoanzisha harakati za
kujikomboa kiuchumi kutoka katika minyororo ya kunyonywa na wakoloni wa kiingereza.
Uchumi wa Zanzibar ulikuwa mikononi mwa wazungu ambao walikuwa wanamiliki njia
zote za uzalishaji mali, wakati waafrika hawakumiliki chochote. Kutokana na
hali hii, Denge na kundi lake wakaamua kuanzisha harakati katika kuwakomboa waafrika
kiuchumi
kwa kuchukua njia kuu za uzalishaji mali kutoka kwa wazungu wachache na
kuziweka mikononi mwa waafrika walio wengi.
Katika
historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi zake, namna yake ya
kufikiri, mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji mali, yaani jinsi uchumi,
uzalishaji, mgawanyo na umilikaji wa mali unavyoendeshwa. Wazo hili la u-marx
limejidhihirisha katika kitabu cha “Mwalimu
Mkuu wa Watu” kana kwamba mfumo
wa uzalishaji mali pamoja na umilikaji
wa mali unavyoendeshwa katika hali ambayo haikuwapa wananchi fursa ya kushiriki
katika maendeleo ya nchi yao jambo lililompelekea
mwalimu
pamoja na wananchi wengine kuanzisha harakati za kuondoa utawala uliopo. Katika
ukurasa wa 8 msanii anasema;
“wananchi walipangwa zefe na
maandamano yalianza
taratibu,
shwari bila vurugu
zozote”.
Maandamano
hayo yalitokana na kasoro zilizopo katika mfumo mzima wa uzalishaji mali
ulivyoendeshwa katika jamii ile.
Pia
katika kitabu cha “morani”
kilichoandikwa na E. Mbogo mwaka 1993 wazo hili la u-marx limejidhihirisha pale ambapo namna ya kufikiri kwa wahusika Jalia, Dongo
na wenzake kulichangiwa na jinsi mfumo wa uzalishaji mali ulivyokuwa
unaendeshwa. Mfumo huo ulikuwa umejaa ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi ndio maana Jalia, Dongo na wenzake
wakaanzisha harakati za mapinduzi. Katika
ukurasa wa 41 mwandishi anasema
“Morani waungane na umma. Waungane kuiendeleza kutafuta nguzo ya uswezi”
Historia
ya mwanadamu huakisi harakati zinazoendelea katika matabaka ya kiuchumi, jamii
au uzalishaji yanayoathiri mabadiliko ya
muundo wa matabaka na hivyo kujitokeza
katika tabaka tawala na tawaliwa ambavyo
huwamo katika mapambano na katika harakati za kugombea uchumi, siasa na faida
za jamii.wazo hili la u-marx linajitokeza katika kitabu hiki pale ambapo
kulikuwa na matabaka kati ya wazungu, wahindi na waafrika kutokana na matabaka
haya kulikuwa na ubaguzi, ilikuwa si rahisi kwa mzungu kuchanganyikana na
mwafrika na vilevile ilikuwa si rahisi kwa mhindi kuchanganyikana na mwafrika. Kwa upande wa makazi, waafrika
waliishi ndani ya vibanda vidogo vidogo vya uswahilini, wakati wazungu na
wahindi waliishi kwenye marosheni na majumba ya watukufu. vilevile kwenye
huduma nyingine waafrika walikwenda kwenye maduka ya mchangani na darajani
ambayo yaliuza bidhaa hafifu, wakati wazungu na wahindi waliingia ndani ya
maduka ya shangani na baghani ambayo yaliuza vitu kwa bei ya ghali na yalitoa
huduma bora za kila namna. Kwa upande wa sehemu za starehe waafrica walistarehe sehemu iitwayo Raha leo,
wazungu walistarehe katika English club na wahindi walistarehe katika Karimjee
club. Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo ya matabaka, Denge pamoja na kundi lake
wakaamua kuanzisha harakati za kutokomeza utawala huo wa kiingereza kwa kutawanya vitabu vyenye mawazo ya
ki-marx.
Historia
ya mwanadamu huakisi harakati zinazoendelea katika matabaka ya uchumi, jamii au
uzalishaji mali yanayoathiri mabadiliko ya muundo wa matabaka na hivyo
kujitokeza katika tabaka tawala na tawaliwa ambavyo huwamo katika mapambano na
katika harakati za kugombea uchumi, siasa na faida za jamii . wazo hili la
u-marx limejidhihirisha katika kitabu cha “Mwalimu
Mkuu wa Watu” pale msanii anapoonesha matabaka katika jamii ile ambapo kuna
tabaka tawala lililoongozwa na mawaziri wa serikali pamoja na raisi, na tabaka
la chini likiongozwa na mwalimu mkuu na wananchi wengine wa tabaka la chini.
Hivyo harakati zilizofanywa na mwalimu mkuu zilikuwa na lengo la kugombea
uchumi, siasa pamoja na faida za kijamii. Katika ukurasa wa 43-44 msanii
anaonesha harakati zilizofanywa na mwalimu
mkuu pindi alipokuwa ameshitakiwa na Fredrick de witts, mwalimu mkuu
aliandika ujumbe kwa wananchi akisema;
“Salamu enyi ndugu
wapendwa Mungu ni mwema. Akikupa chakula kigumu, hukupa pia na meno
magumu.Nawatumieni msaidizi atakayewatia faraja na kuwaelekeza yote ambayo
ningewaelekeza. Msikilizeni na mfuate maelekezo yake nanyi hamtakuwa yatima
tena: eleweni kuwa njia ya ushindi ni ngumu, lakini jipeni moyo kwa maana siku
ya ushindi iko karibu. Usiku mzito ni pale karibu na kucha. Ni mimi ndugu yenu
Ngowe Boniface.
Vilevile katika kitabu cha “Morani” kimeelezea suala ya matabaka mfano tabaka la juu la wenye
pesa ambalo ndilo linalomiliki njia kuu za uzalishaji mali liliwahusisha
mhusika Nungunungu na Mlemeta, na tabaka la chini ambalo lilikuwa likinyanyaswa
na tabaka la juu kupitia vyombo vya dola likiwahusisha wahusika kama Jalia,
Dongo na wenzake. Hivyo ikawapelekea wahusika hao wa tabaka la chini kuanzisha
harakati dhidi ya kupambana na tabaka tawala ili kuleta ukombozi katika tabaka
la chini ili kugombea uchumi, siasa na faida za jamii. Katika uk. 66, mwandishi
anaonesha jinsi vyombo vya sheria vinavyowatendea watu wa tabaka la chini kutokana na kutokuwa na sauti yoyote katika jamii.
Ulazini wa binadamu umeundwa na itikadi, thamani ya
kitu na namna ya kufikiri na kuhisi ni kupitia hivi, mwanadamu huona ulimwengu
wake nay ale anayoyaona na hayo
yanayomzunguka kuwa ni ukweli. Wazo hili la u-marx linajitokeza katika kitabu
hiki, kwa kitendo cha Denge na kundi lake kugundua kuwa wananyonywa, wanaonewa
na kugandamizwa na wakoloni ulikuwa ni ukombozi wa kifikra ndio maana
walianzisha harakati za kudai haki zao za msingi. Pia kitendo cha Yasmini kuona
kuwa baadhi ya mila na desturi zinamnyanyasa mwanamke na kuamua kuachana nazo
inadhihirisha wazi kuwa Yasmini alikuwa na uwezo wa kufikiri na kuona mbali.
Ulazini wa binadamu umeundwa na itikadi, thamani ya
kitu na namna ya kufikiri na kuhisi ni kupitia hivi, mwanadamu huona ulimwengu
wake nay ale anayoyaona na hayo yanayomzunguka kuwa ukweli. Wazo hili la u-marx
limejidhihirisha katika kitabu hiki cha “Mwalimu
Mkuu wa Watu” kwa kuwa msanii anamchora mwalimu mkuu kwa jinsi ambavyo
namna yake ya kufikiri, kuhisi pamoja na utashi wa hali ya juu ndio uliomfanya
kuona uovu uliokuwa ukitendeka katika tabaka tawala. Uovu huo ni pamoja na
serikali kuruhusu wawekezaji uchwara ambao hawakuwa na tija yoyote kwa wananchi
walio wengi pamoja na rushwa iliokithiri miongoni mwa viongozi wakubwa wa nchi,
na ndicho kitu kilichompelekea mwalimu mkuu kuanzisha harakati dhidi ya tabaka
tawala.
Pia katika kitabu cha “kilio chetu” kilichoandikwa na Medical Aid Foundation, wazo hili la
u-marx limejidhihirisha pale ambapo
msanii amemtumia mhusika mjomba , ambaye aliona kuwa ni muhimu kuwapa watoto
elimu ya kijinsia, lakini jamii iliona kuwa kuwapa watoto elimu ya kijinsia ni
kuwafundisha watoto kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo kitu ambacho si
sahii.
Ubepari kama njia ya uzalishaji mali unatabiriwa na
kuvunjiliwa mbali kutokana na juhudi za wafanyakazi au utaishia wenyewe
kutokana na mbegu za maangamizo zilizosheheni. Wazo hili la u-marx
linajidhihirisha katika kitabu hiki cha “Vuta
n’kuvute” pale ambapo harakati za Denge na kundi lake kutawanya vitabu na
magazeti yaliyokuwa yakipinga siasa ya ukoloni wa kiingereza. Pia Denge
alisomeshwa na waingereza na huyo ndiye aliyekuja kupinga utawala wa kiingereza ambapo alipata
elimu na hiyo elimu ilimsaidia ndio maana akaanzisha harakati za kupinga
serikali ya kikoloni.
Ubepari kama njia ya uzalishaji mali unatabiliwa na
kuvunjiliwa mbali kutokana na juhudi za wafanyakazi au utaishia wenyewe
kutokana na mbegu za maangamizo zilizosheheni. Wazo hili la ki-marx
linajidhihirisha katika kitabu cha “Mwalimu
Mkuu wa Watu” kwani mwandishi anaonesha mbegu za maangamizo zilizopandwa na
serikali kwa kuwapa elimu mwalimu mkuu wanajeshi pamoja na wanafunzi ambapo
kutikana na uovu uliofanywa na serikali ulimfanya mwalimu mkuu pamoja na
wananchi kuwa na upeo wa kuyaona maovu hayo na hivyo kuanzisha harakati dhidi
ya uovu huo.
Wazo hili la umarx pia limejidhihirisha katika kitabu
cha “ kivuli kinaishi” kilichoandikwa na Said A. Mohamed, pale ambapo
ubepari uliokuwepo dhidio ya serikali ya
Bi kirembwe ndio uliopelekea kuvunjiliwa
mbali kwa utawala wake kupitia wahusika Mtolewa wali na wengineo ambao walikuwa
wafanyakazi wa tabaka la chini ambao walikuwa wakigandamizwa katika nyanja zote
za kimaisha mfano kichumi kisiasa na kijamii. Katika uk. wa 70 msanii anasema;
“Hamtaweza kufahamu mpaka niwatoeni
mzigo mlionao …
hamtatambua mpaka nikufumbueni macho na kukuzibueni masikio…”
Mtolewa
aliwafumbua macho wali wenzake kwa kuwalisha unga wa rutuba elimu inayomfanya
mtu ajitambue na atambue nafasi yake katika jamii na aweze na kuwaelimisha
wenzake.
Njia
za kusaidia na labda hata kuharakisha kuangamizwa kwa ubepari ni kudadisi, kukosoa,
kushutumu, kulaumu na kufichua ukatili uliopo katika itikadi ya kibwenyenye
inayouimarisha ubepari. Wazo hili la u-marx linajidhihirisha katika kitabu hiki
pale ambapo Denge na kundi lake walipoandaa vipeperushi na maandamano ya
kushutumu, kudadisi, kukosoa, kulaumu na kufichua ukatili uliopo katika
serikari ya kikoloni. Denge alikuwa mwanaharakati wa kupinga utawala wa
mwingereza visiwani Unguja na Pemba na
katika harakati zake alisambaza vitabu vya Karlmarx, magazeti yanayopinga ukoloni
pamoja na makaratasi ya uchochezi dhidi ya makoloni hayo.
Njia
za kusaidia na labda hata kuharakisha kuangamizwa kwa ubepari ni kudadisi,
kukosoa, kushutumu, kulaumu na kufichua ukatili uliopo katika itikadi ya kibwenyenye inayouimarisha
ubepari. Wazo hili limethibitishwa katika kitabu hiki cha “Mwalimu Mkuu wa Watu” kwani msanii amemchora mwalimu mkuu kwa jinsi
ambavyo alikosoa, alilaumu na kufichua ubatili uliofanywa katika serikali hiyo,
ubatili huo ni pamoja na kuruhusu wawekezaji wasio na tija katika nchi, vilevile
rushwa iliyokithiri miongoni mwa viongozi wakubwa wa nchi.
Pia
katika kitabu cha Kivuli kinaishi wazo hili la u-marx limejitokeza pale ambapo
mwandishi amemtumia mhusika Mtolewa
alipowalisha wari unga wa rutuba
kwa lengo la kukosoa, kushutumu, kulaumu na kufichua ubatili uliokuwepo
katika serikali ya Bi kirembwe katika jamii ya Giningi.
Nadharia ya ki-marx inahusishwa na kuandamana
pamoja na hata kuelezeka kwa matendo ya
utekelezaji dhidi ya mfumo mzima wa kibepari. Wazo hili la ki-marx linajidhihirisha
katika kitabu hiki pale ambapo Denge na kundi lake walipoamua kuanzisha
maandamano makubwa na Denge alikuwa mstari wa mbele akiwa na makaratasi
aliyokuwa anayagawa kwa mtu yoyote aliyemkaribia. Makaratasi hayo yalikuwa
yanapinga ukoloni ambao ulikuwa unawanyonya na kuwagandamiza watu wa tabaka la
chini.
Nadharia
ya ki-marx inahusishwa na kuandamana pamoja na hata kuelezeka kwa matendo ya
utekelezaji dhidi ya mfumo mzima wa kibepari. Wazo hili la u-marx limejitokeza
katika kitabu hiki, pale ambapo mwalimu mkuu aliongoza maandamano pamoja
nawananchi wengine dhidi ya uovu uliotendwa na viongozi wa serikali.mfano
katika ukurasa wa 8 msanii anasema;
“ maandamano
hayo yalijumuisha watoto, vijana, wazee, akina mama na hata vilema na ulemavu wao. Waliendelea mbele na kukata
kushoto kuingia katika barabara iendayo mojo kwa moja kiwandani.”
Katika
kitabu cha Morani wazo hili la u-marx limejidhihirisha pale ambapo mtunzi
amewatumia wahusika Jalia, Dongo na
wenzake walivyokuwa mstari wa mbele katika kupiga vita uhujumu uchumi, kuandaa maandamano
yaliyolenga kupambana na mfumo mzima wa serikani iliopo madarakani uliokuwa umejaa rushwa, uhujumu uchumi na
uongozi mbaya. Katika uk.41 msanii anasema;
“Morani waungane na umma kuiendeleza kutafuta nguzo ya uswezi”
No comments:
Post a Comment