Friday, 12 February 2016

SARUFI YA KISWAHILI HAIJIEGEMEZI KATIKA SARUFI YA KIINGEREZA

B. F. KIWALE
P.O BOX 774
IRINGA


© Kiwale, F. Brasto 2015


ISBN 9976 911 49 1




chapa ya kwanza 2015, December. 28.

Haki zote zimehifadhiwa. hakuna sehemu ya kazi hii itakayo ruhusiwa kuirudia kuitengeneza, kwa namna yoyote ile, bila ruhusa ya mwandishi au B. F  Consult P.O. Box 774, IRINGA.




Printing and publishing consultancy by
Kiwale Associates/ TFC, P.O Box 326,


Iringa, Tanzania.


Maana ya sarufi
 Sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na matumizi yake ambayo kwa kawaida  hukubalika kwa watumiaji wake (gaynor 1968:88 katika kihore na wenzake 2008).
Sarufi ni kanuni za lugha zinazo mwezesha mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha (Besha 2007).
 Kwa ujumla Sarufi ni sheria au kanuni zinazo paswa kufuatwa katka lugha fulani. Kila lugha huwa na kanuni na sheria zake, sheria za lugha zimegawanyika katika makundi manne yanayo julikana kama matawi ya sarufi yaani sarufi matamshi, maumbo, muundo na maana.
Sio kweli kwamba sarufi ya Kiswahili inajiegemeza katika sarufi ya kiingereza hii ni kwa sababu kila lugha ina kanuni, sheria na taratibu zake ambazo ndizo huzingatiwa na watumiaji wa lugha hiyo kwa ufasaha, uzingatiaji wa matumizi ya luhgha ya Kiswahili katika vipengere hivyo huweza kuwa na tofauti kubwa kutoka katika lugha kiingereza kama ifuatavyo;
Sarufi ya Kiswahili na kingereza hutofautiana katika mpangilio wa maneno au uhusiano wa maneno katika kuunda tungo za lugha husika, kwa mfano katika Kiswahili mara nyingi tunaanza na nomino na kufuata kategoria zingine zinazoweza zikaukilia uhusiano wa kiasili wa lugha wa lugha ya Kiswahili, kwa mfano; mtoto mdogo. Lakini katika kingereza huweza kuanza na hata kivumishi kisha kufuatiwa na nomino kama, kileines kind. Hivyo basi sarufi ya kingereza si sawa na sarufi ya kingereza. Muundo wa sentensi, katika sarufi ya Kiswahili mara nyingi huwa N+ V+T+E. mfano;
 Mtoto mzuri anacheza uwanjani.
  N        V          T             E
 Katika muundo wa sentensi za kiingereza huanza na kivumishi. mfano,
A beautiful girl playing on the ground.
    Adj           N
Hivyo mara nyingi sentensi za Kiswahili tunaanza na Nomino wakati katika kiindereza zinaanza na kivumishi badala ya kuanza na Nomino. Hivyo sarufi ya Kiswahili inajitegema haijajiegemeza katika sarufi ya kiingereza, kwni kama muundo wa sentensi za Kiswahili ungekuwa umejiegemeza katika muundo wa kiingereza ingekuwa, mzuri mtoto anacheza uwanjani (Khamisi, 2002).
Tabia za vitenzi vya Kiswahili ni tofauti na tabia ya vitenzi vya kingereza kwa mfano kitenzi cha Kiswahili huweza kuundwa na nafsi, njeo, yambwa na yambiwa, mzizi na kiambishi(viambishi tamati) kwa wakati mmoja ili hali vitenzi vya kingereza  si rahisi kuwa na muundo huo, Kwa mfano;
i). A+na +m +chez+ e+ a
    1    2     3      4      5   6
1-      Inaonesha nafsi ya tatu umoja
2-      Inainesha na njeo ya wakati uliopo
3-      Inaonesha yambwa
4-      Inaonesha mzizi wa kitenzi
5-      Huonesha hali ya kutendea
6-      Kiambishi tamati maana
Kiingereza “He is playing for him” hivyo ni dhahili kuwa muundo wa tungo namba moja na mbili ni tofauti ili hali zina maana moja.
Kanuni za utamshi wa sauti (fonimu) za lugha ya kingereza na ile ya Kiswahili ni tofauti, kwa mfano fonimu “a” hutamkwa kama /a/ kifonetiki lakini katika kiingereza ina sauti mbali mbali kutegemeana na mahali ilipo katika mpangilio wa neno, kwa mfano;
i-seat /si:t/
e-set/set/
ae-sat /sᶕe/
a-march /maits/
a-away /a’weI/ (Swan 2006)
Tofauti ya viambishi na matumizi kati ya sarufi ya Kiswahili na sarufi ya kingereza, kwa mfano hakuna kiambishi “n” cha wingi katika sarufi ya kingereza ambacho kipo katika sarufi ya Kiswahili na kina matumizi anuai kama asemavyo ashton(1994:2) na Palome(1967:113) katika Mukama(2000:181): Dhima ya kwanza ni kueleza tungo amri zinazo amrisha watu wengi kwa mfano;
1.      A)  Pikeni
b)      Ondoeni visu
Dhima ya tatu ni utatuzi wa utata wa kimaandishi “wa” ambacho kinawakilisha nafsi ya pili na ya tatu -ni hutokea tu kuhusiana na nafsi ya pili, kwa hiyo tungo namba (2) haina utata
2. Nitawaombeni
Tabia za maneno katika lugha ya Kiswahili na kiingereza ni tofauti kwa mfano miishio ya maneno katika sarufi ya Kiswahili mara nyingi huishia na irabu tofauti na miishio ya ya maneno katika sarufi ya kiingereza ambayo huweza kuishia na konsonati (Shayo, 200:95-104), katika swahili grammar, ameainisha maneno mengi ya lugha ya kisarufi na maneno hayo yote yanaishia na irabu (a, e, i, o, u). Katika kiingereza irabu mara nyingi ndiyo huishia, Mfano; talk, refresh, look.
Kuna baadhi ya vitenzi vya kingereza hufuata aruzi ya umoja na wingi ili hali vitenzi hivyohivyo katika lugha ya Kiswahili havifuati arudhi hiyo kwa mfano;
Kingereza                                                                               kiswahili
Singular    prular                                                            umoja                wingi
-plate         plates                                                            sahani                  sahani
Kanuni za kupangilia maneno katika kuunda sentensi za Kiswahili na kiingereza ni tofauti kwa mfano; katika Kiswahili unaweza kuhusianisha/ kufasiri sentensi ya kiingereza kwenda kwenye sarufi ya Kiswahili bila kuangalia maana ya jumla na ikawa na mpangilio sahihi au isilete maana, kama katika sentensi zifuatazo;
Kingereza                                       Kiswahili
(i)                 When will he dig for him?                   Atamlima lini?
(ii)               When will he dig for him?                   Atalima lini?
Sentensi ya kwanza ya (i) na (ii) zina mpangilio sahihi lakini zimeathiriwa na sarufi Ya kiingereza na kuleta maana tata katika lugha ya Kiswahili hivyo zinapaswa kufasiriwa bila kuegemea katika sarufi ya kiingereza ili kuleta maana kama, Atalimia lini? (Mkama 2000:26).
Sintakisia ya Kiswahili ina michakato anuai tofauti na ile iliyoko katika sintakisia ya ya kingereza, kwa mfano katika sintakisia ya Kiswahili kuna michakato ya kimofo-sintaksia, Vitale (1981) kama alivyo nukuliwa na Mukama (2000:181) anasema “lugha ya Kiswahili kama ilivyo katika lugha nyingine za kibantu, ina alama mbalimbali zenye kuashilria michakato tofauti ya kinsintaksia ya kiuamilifu, kwa mfano viambishi kiima na yambwa, sintaksia ya miundo kama vile (kutendewa, kutendeka) na mabadiliko ya uelekezi asilia (mathalani, kutendea na kutendesha) anaendelea kusema kuwa viambishi tamati vya vitenzi hasa ndivyo vinavyo husika sana kisintaksia na kila kiambishi hukalia michakato ya kisintaksia.
Katika ukanushi, katika muundo wa sarufi ya Kiswahili kwenye sentensi ukanushi hupatikana katika neno zima lakini si kama kipande cha neno ndicho huonesha ukanushi, mfano
            Juma hatakuja darasani leo
Hivyo ukanushi huo unaonesha upo katika neno moja lenye ukanushi lakini si kama kipande fulani ndicho kinachoonesha ukanushi kama ilivyo katika muundo wa kiingereza, mfano
            Juma will not come to the classroom today.
Neno “NOT” linaonesha ukanushi lakini ni maneno tofauti na kitenzi, wakati katika Kiswahili ukanushi umeunganishwa na kitenzi (Habwe & na wenzake, 2007).
Katika kipengele cha wakati, katika Kiswahili kiambishi cha wakati huamabatana na kitenzi, mfano
            Mvulana mtanashati atakuja kesho.
Katika kiingereza,
            A handsome boy will come tomorrow.
Katika sentensi ya Kiswahili “ta” ndiyo kiambishi kinachowakilisha njeo ya wakati ujao, lakini katika sentensi ya kiingereza “will” ndiyo inayowakilisha njeo ya wakati ujao. Katika sentensi ya Kiswahili imeambatanishwa pamoja na kitenzi, hivyo sarufi ya Kiswahili inajitegemea haijiegemezi katika sarufi ya kiingereza (Gofkosoft, 2009).
Katika maumbo ya umoja na wingi, maumbo ya umoja na wingi katika sarufi ya Kiswahili huweza kujitokeza mwanzoni mwa neno, mfano
            Umoja                                                 wingi
            Kiti                                                      viti
            Meza                                                     Ø
Lakini katika sentensi za kiingereza wingi unapatikana mwishoni mwa neno, mfano;
            Singular                                                          plural 
            Chair                                                               chairs
Table                                                               tables
Hivyo sarufi ya Kiswahili inajitegemea kwani maumbo katika umoja na wingi yanatofautiana na yale ya kiingereza, hivyo kila sarufi inajitegemea.
Katika fonolojia, uamilifu wa fonimu za Kiswahili ni tofauti na uamilifu wa fonimu za kiingereza. Hoja hii inashadadiwa na (Mgullu, 1999: 56) aliyesema uamilifu wa fonimu katika lugha ni wa kipekee.kwa lugha hiyohiyo tu na haufanani kabisa na uamilifu wa fonimu za lugha huzingatia hata kama fonimu hizo zinafanana kifonetiki. Kwa mfano, Kiswahili kina fonimu [i] na kiingereza pia kinayo fonimu [i] na zote zinafanana kifonetiki, lakini hii haina maana kuwa mtumizi ya irabu hizi katika lugha ya Kiswahili na kiingereza yanafanana kwa hoja hii ni dhahiri kuwa Kiswahili kinajiegemeza kisarufi. Pia kwa upande wa matumizi ya irabu utaona kwamba irabu za Kiswahili hutumiwa zaidi kuliko irabu za lugha ya kiingereza. Hii inatokana na tofauti za miundo ya silabi katika luga hizi mbili. Ambapo silabi za Kiswahili karibia zote lazima ziishie na irabu mfano ba, ma, cha, mbu, ngo, ngwe, mwa. Tofauti na kiingereza ambapo silabi zake nyingi haziishii na iarbu (mgullu, 1999: 55). Hivyo Kiswahili kinajitegemea kisarufi.
Lugha ya Kiswahili huzihusu konsonati chache kuwa silabi katika maneno. Hizi ni nazali /m/ na /n/. hizi nazo huwa silabi katika mazingira maalumu tu na si lazima ziwe silabi muda wote, mfano katika maneno kama mpaka, mtu, alimpiga, nchi, nta (mgullu, 1999:74).
Katika uambishaji, Kiswahili ni lugha ambishi bainishi ambapo viambishi na mzizi huwa havichangavyiki kabisa na mtu anaweza kuonyesha kwa urahisi kabisa mizizi ipi na viambishi vipi. Kwa mfano; katika maneno yafuatayo sehemu zilizopigiwa mastari ni mzizi M-toto, Ma-cho, a-na-pig-a, a-na-chez-a, a-li-ku-j-a na nakadhalika. Lakini kiingereza ni lugha ambishi mchanganyiko kwamba, baada ya neno kuambishwa viambishi huchanganyika na mzizi na inakuwa ni vigumu kutambua mzizi ni upi na viambishi bi vipi. Tazama mfano; katika manno yafuatayo; Mice (wingi wa mouse), came (njeo iliyopita ya come), went (njeo iliyopita ya go), gave (njeo iliyopita ya give) (Mgullu, 1999: 12-13). Hivyo kwa mafno huu ni dhahiri kuwa Kiswahili kina sarufi inayojitegemea na sio kujiegemeza katika lugha ya kiingereza.
Utofauti katika mkazo wakati wa utamkaji wa maneno (Mgullu, 1999:37) anasema kila lugha huwa na utaratibu wake wa kuweka mkazo katika maneno ya lugha hiyo, lugha zingine mahali pa mikazo katika maneno yao haibadiliki, mfano lugha ya Kiswahili maneno yake huwekewa mikazo katika silabi ya pili kutoka mwisho, mfano; Mjomba, lakini lugha zingine zina taratibu zao za kuweka mikazo, mafano kiingereza kina mkazo huru kwamba neno huweza kuwekewa mkazo mahali popote.
Ujinsia, katika sarufi ya Kiswahili hakuna ujinsia bali hujidhihisha kwa kutaja jina moja kwa moja la mtu, yaani kutaka kuonesha kuwa anayezungumzwa ni mwanamke au ni mwanaume/ mvulana au msichana, mfano;
Ø Analima shamba vizuri sana.
Katika sentensi hiyo hapo juu haijaonesha anayelima ni wa kike au wa kiume, hivyo kuna uhitaji wa mhusika, lakini katika sarufi ya kiingereza kuna ujinsia kwa mwanzoni mwa sentensi lazima ujinsia uoneshwe kuwa ni wakike au wa kiume, mfano;
                                    She is cultivating a farm nicely.
Hivyo katika sentensi hapo juu inaonyesha ujinsia kuwa anayelima ni wa kike wakati sentensi ya Kiswahili bado ilikuwa na swali kuwa anayelima ni mwanaume au mwanamke. Hivyo lugha zote mbili yaani kiingereza na Kiswahili sarufi yake inajitemea kama ilivyojidhihirisha katika mifano ya sentensi hapo juu
Kwa ujumla kila lugha huwa na utaratibu na kanuni zake katika kupanga maneno na kuunda sentensi na mpangilio, hii inaweza kukaribiana kwa lugha za jamii moja kwa moja na pia ukatofautiana sana na lugha za jamii tofauti, kwa kuona kuwa kila lugha huwa ina utaratibu wake na kanuni zake ni dhahiri. Hivyo lugha ya Kiswahili inajitegemea katika sarufi yake na siyo inajiegemeza katika sarufi ya kiingereza, kwani Kiswahili ni lugha inayojitoshereza kimaana a katika ubora wake japokuwa ina ukaribu na lugha zingine kama kiingereza na kibantu pia.

                                                                

2 comments: