Friday, 12 February 2016
SARUFI YA KISWAHILI HAIJIEGEMEZI KATIKA SARUFI YA KIINGEREZA
B. F. KIWALE
P.O BOX 774
IRINGA
© Kiwale, F. Brasto 2015
ISBN 9976 911 49 1
chapa ya kwanza 2015, December. 28.
Haki zote zimehifadhiwa. hakuna sehemu ya kazi hii itakayo ruhusiwa kuirudia kuitengeneza, kwa namna yoyote ile, bila ruhusa ya mwandishi au B. F Consult P.O. Box 774, IRINGA.
Printing and publishing consultancy by
Kiwale Associates/ TFC, P.O Box 326,
Iringa, Tanzania.
Maana
ya sarufi
Sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na
sheria, kanuni na matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake (gaynor 1968:88
katika kihore na wenzake 2008).
Sarufi
ni kanuni za lugha zinazo mwezesha mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye
kukubaliwa na wazawa wa lugha (Besha 2007).
Kwa ujumla Sarufi ni sheria au kanuni zinazo
paswa kufuatwa katka lugha fulani. Kila lugha huwa na kanuni na sheria zake,
sheria za lugha zimegawanyika katika makundi manne yanayo julikana kama matawi
ya sarufi yaani sarufi matamshi, maumbo, muundo na maana.
Sio
kweli kwamba sarufi ya Kiswahili inajiegemeza katika sarufi ya kiingereza hii
ni kwa sababu kila lugha ina kanuni, sheria na taratibu zake ambazo ndizo
huzingatiwa na watumiaji wa lugha hiyo kwa ufasaha, uzingatiaji wa matumizi ya
luhgha ya Kiswahili katika vipengere hivyo huweza kuwa na tofauti kubwa kutoka
katika lugha kiingereza kama ifuatavyo;
Sarufi
ya Kiswahili na kingereza hutofautiana katika mpangilio wa maneno au uhusiano
wa maneno katika kuunda tungo za lugha husika, kwa mfano katika Kiswahili mara
nyingi tunaanza na nomino na kufuata kategoria zingine zinazoweza zikaukilia
uhusiano wa kiasili wa lugha wa lugha ya Kiswahili, kwa mfano; mtoto mdogo.
Lakini katika kingereza huweza kuanza na hata kivumishi kisha kufuatiwa na
nomino kama, kileines kind. Hivyo basi sarufi ya kingereza si sawa na sarufi ya
kingereza. Muundo wa sentensi, katika sarufi ya Kiswahili mara nyingi huwa N+
V+T+E. mfano;
Mtoto mzuri anacheza
uwanjani.
N V T
E
Katika muundo
wa sentensi za kiingereza huanza na kivumishi. mfano,
A beautiful girl
playing on the ground.
Adj N
Hivyo
mara nyingi sentensi za Kiswahili tunaanza na Nomino wakati katika kiindereza
zinaanza na kivumishi badala ya kuanza na Nomino. Hivyo sarufi ya Kiswahili
inajitegema haijajiegemeza katika sarufi ya kiingereza, kwni kama muundo wa
sentensi za Kiswahili ungekuwa umejiegemeza katika muundo wa kiingereza
ingekuwa, mzuri mtoto anacheza uwanjani (Khamisi, 2002).
Tabia
za vitenzi vya Kiswahili ni tofauti na tabia ya vitenzi vya kingereza kwa mfano
kitenzi cha Kiswahili huweza kuundwa na nafsi, njeo, yambwa na yambiwa, mzizi
na kiambishi(viambishi tamati) kwa wakati mmoja ili hali vitenzi vya
kingereza si rahisi kuwa na muundo huo,
Kwa mfano;
i). A+na
+m +chez+ e+ a
1
2 3 4
5 6
1-
Inaonesha
nafsi ya tatu umoja
2- Inainesha
na njeo ya wakati uliopo
3- Inaonesha
yambwa
4- Inaonesha
mzizi wa kitenzi
5- Huonesha
hali ya kutendea
6- Kiambishi
tamati maana
Kiingereza
“He is playing for him” hivyo ni dhahili kuwa muundo wa tungo namba moja na
mbili ni tofauti ili hali zina maana moja.
Kanuni
za utamshi wa sauti (fonimu) za lugha ya kingereza na ile ya Kiswahili ni
tofauti, kwa mfano fonimu “a” hutamkwa kama /a/ kifonetiki lakini katika kiingereza
ina sauti mbali mbali kutegemeana na mahali ilipo katika mpangilio wa neno, kwa
mfano;
i-seat
/si:t/
e-set/set/
ae-sat
/sᶕe/
a-march
/maits/
a-away
/a’weI/ (Swan 2006)
Tofauti
ya viambishi na matumizi kati ya sarufi ya Kiswahili na sarufi ya kingereza,
kwa mfano hakuna kiambishi “n” cha wingi katika sarufi ya kingereza ambacho
kipo katika sarufi ya Kiswahili na kina matumizi anuai kama asemavyo
ashton(1994:2) na Palome(1967:113) katika Mukama(2000:181): Dhima ya kwanza ni
kueleza tungo amri zinazo amrisha watu wengi kwa mfano;
1. A)
Pikeni
b) Ondoeni
visu
Dhima
ya tatu ni utatuzi wa utata wa kimaandishi “wa” ambacho kinawakilisha nafsi ya
pili na ya tatu -ni hutokea tu kuhusiana na nafsi ya pili, kwa hiyo tungo namba
(2) haina utata
2.
Nitawaombeni
Tabia
za maneno katika lugha ya Kiswahili na kiingereza ni tofauti kwa mfano miishio
ya maneno katika sarufi ya Kiswahili mara nyingi huishia na irabu tofauti na
miishio ya ya maneno katika sarufi ya kiingereza ambayo huweza kuishia na
konsonati (Shayo, 200:95-104), katika swahili grammar, ameainisha maneno mengi
ya lugha ya kisarufi na maneno hayo yote yanaishia na irabu (a, e, i, o, u). Katika
kiingereza irabu mara nyingi ndiyo huishia, Mfano; talk, refresh, look.
Kuna
baadhi ya vitenzi vya kingereza hufuata aruzi ya umoja na wingi ili hali
vitenzi hivyohivyo katika lugha ya Kiswahili havifuati arudhi hiyo kwa mfano;
Kingereza kiswahili
Singular prular umoja wingi
-plate plates
sahani sahani
Kanuni
za kupangilia maneno katika kuunda sentensi za Kiswahili na kiingereza ni tofauti
kwa mfano; katika Kiswahili unaweza kuhusianisha/ kufasiri sentensi ya
kiingereza kwenda kwenye sarufi ya Kiswahili bila kuangalia maana ya jumla na
ikawa na mpangilio sahihi au isilete maana, kama katika sentensi zifuatazo;
Kingereza Kiswahili
(i)
When will he dig for him? Atamlima lini?
(ii)
When will he dig for him? Atalima lini?
Sentensi
ya kwanza ya (i) na (ii) zina mpangilio sahihi lakini zimeathiriwa na sarufi Ya
kiingereza na kuleta maana tata katika lugha ya Kiswahili hivyo zinapaswa
kufasiriwa bila kuegemea katika sarufi ya kiingereza ili kuleta maana kama,
Atalimia lini? (Mkama 2000:26).
Sintakisia
ya Kiswahili ina michakato anuai tofauti na ile iliyoko katika sintakisia ya ya
kingereza, kwa mfano katika sintakisia ya Kiswahili kuna michakato ya kimofo-sintaksia,
Vitale (1981) kama alivyo nukuliwa na Mukama (2000:181) anasema “lugha ya
Kiswahili kama ilivyo katika lugha nyingine za kibantu, ina alama mbalimbali
zenye kuashilria michakato tofauti ya kinsintaksia ya kiuamilifu, kwa mfano
viambishi kiima na yambwa, sintaksia ya miundo kama vile (kutendewa, kutendeka)
na mabadiliko ya uelekezi asilia (mathalani, kutendea na kutendesha) anaendelea
kusema kuwa viambishi tamati vya vitenzi hasa ndivyo vinavyo husika sana
kisintaksia na kila kiambishi hukalia michakato ya kisintaksia.
Katika
ukanushi, katika muundo wa sarufi ya Kiswahili kwenye sentensi ukanushi
hupatikana katika neno zima lakini si kama kipande cha neno ndicho huonesha
ukanushi, mfano
Juma hatakuja darasani leo
Hivyo
ukanushi huo unaonesha upo katika neno moja lenye ukanushi lakini si kama
kipande fulani ndicho kinachoonesha ukanushi kama ilivyo katika muundo wa
kiingereza, mfano
Juma will not come to the
classroom today.
Neno
“NOT” linaonesha ukanushi lakini ni maneno tofauti na kitenzi, wakati katika
Kiswahili ukanushi umeunganishwa na kitenzi (Habwe & na wenzake, 2007).
Katika
kipengele cha wakati, katika Kiswahili kiambishi cha wakati huamabatana na
kitenzi, mfano
Mvulana mtanashati atakuja
kesho.
Katika
kiingereza,
A handsome boy will come
tomorrow.
Katika
sentensi ya Kiswahili “ta” ndiyo kiambishi kinachowakilisha njeo ya wakati
ujao, lakini katika sentensi ya kiingereza “will” ndiyo inayowakilisha njeo ya
wakati ujao. Katika sentensi ya Kiswahili imeambatanishwa pamoja na kitenzi,
hivyo sarufi ya Kiswahili inajitegemea haijiegemezi katika sarufi ya kiingereza
(Gofkosoft, 2009).
Katika
maumbo ya umoja na wingi, maumbo ya umoja na wingi katika sarufi ya Kiswahili
huweza kujitokeza mwanzoni mwa neno, mfano
Umoja
wingi
Kiti viti
Meza Ø
Lakini
katika sentensi za kiingereza wingi unapatikana mwishoni mwa neno, mfano;
Singular plural
Chair chairs
Table tables
Hivyo
sarufi ya Kiswahili inajitegemea kwani maumbo katika umoja na wingi yanatofautiana
na yale ya kiingereza, hivyo kila sarufi inajitegemea.
Katika
fonolojia, uamilifu wa fonimu za Kiswahili ni tofauti na uamilifu wa fonimu za
kiingereza. Hoja hii inashadadiwa na (Mgullu, 1999: 56) aliyesema uamilifu wa
fonimu katika lugha ni wa kipekee.kwa lugha hiyohiyo tu na haufanani kabisa na
uamilifu wa fonimu za lugha huzingatia hata kama fonimu hizo zinafanana
kifonetiki. Kwa mfano, Kiswahili kina fonimu [i] na kiingereza pia kinayo
fonimu [i] na zote zinafanana kifonetiki, lakini hii haina maana kuwa mtumizi
ya irabu hizi katika lugha ya Kiswahili na kiingereza yanafanana kwa hoja hii
ni dhahiri kuwa Kiswahili kinajiegemeza kisarufi. Pia kwa upande wa matumizi ya
irabu utaona kwamba irabu za Kiswahili hutumiwa zaidi kuliko irabu za lugha ya
kiingereza. Hii inatokana na tofauti za miundo ya silabi katika luga hizi
mbili. Ambapo silabi za Kiswahili karibia zote lazima ziishie na irabu mfano
ba, ma, cha, mbu, ngo, ngwe, mwa. Tofauti na kiingereza ambapo silabi zake
nyingi haziishii na iarbu (mgullu, 1999: 55). Hivyo Kiswahili kinajitegemea
kisarufi.
Lugha
ya Kiswahili huzihusu konsonati chache kuwa silabi katika maneno. Hizi ni
nazali /m/ na /n/. hizi nazo huwa silabi katika mazingira maalumu tu na si
lazima ziwe silabi muda wote, mfano katika maneno kama mpaka, mtu, alimpiga,
nchi, nta (mgullu, 1999:74).
Katika
uambishaji, Kiswahili ni lugha ambishi bainishi ambapo viambishi na mzizi huwa
havichangavyiki kabisa na mtu anaweza kuonyesha kwa urahisi kabisa mizizi ipi
na viambishi vipi. Kwa mfano; katika maneno yafuatayo sehemu zilizopigiwa
mastari ni mzizi M-toto, Ma-cho, a-na-pig-a, a-na-chez-a,
a-li-ku-j-a na nakadhalika. Lakini kiingereza ni lugha ambishi
mchanganyiko kwamba, baada ya neno kuambishwa viambishi huchanganyika na mzizi
na inakuwa ni vigumu kutambua mzizi ni upi na viambishi bi vipi. Tazama mfano;
katika manno yafuatayo; Mice (wingi wa mouse), came (njeo iliyopita ya come),
went (njeo iliyopita ya go), gave (njeo iliyopita ya give) (Mgullu, 1999:
12-13). Hivyo kwa mafno huu ni dhahiri kuwa Kiswahili kina sarufi
inayojitegemea na sio kujiegemeza katika lugha ya kiingereza.
Utofauti
katika mkazo wakati wa utamkaji wa maneno (Mgullu, 1999:37) anasema kila lugha
huwa na utaratibu wake wa kuweka mkazo katika maneno ya lugha hiyo, lugha
zingine mahali pa mikazo katika maneno yao haibadiliki, mfano lugha ya
Kiswahili maneno yake huwekewa mikazo katika silabi ya pili kutoka mwisho,
mfano; Mjomba, lakini lugha zingine zina taratibu zao za kuweka mikazo,
mafano kiingereza kina mkazo huru kwamba neno huweza kuwekewa mkazo mahali
popote.
Ujinsia,
katika sarufi ya Kiswahili hakuna ujinsia bali hujidhihisha kwa kutaja jina
moja kwa moja la mtu, yaani kutaka kuonesha kuwa anayezungumzwa ni mwanamke au
ni mwanaume/ mvulana au msichana, mfano;
Ø Analima shamba vizuri sana.
Katika
sentensi hiyo hapo juu haijaonesha anayelima ni wa kike au wa kiume, hivyo kuna
uhitaji wa mhusika, lakini katika sarufi ya kiingereza kuna ujinsia kwa
mwanzoni mwa sentensi lazima ujinsia uoneshwe kuwa ni wakike au wa kiume,
mfano;
She
is cultivating a farm nicely.
Hivyo
katika sentensi hapo juu inaonyesha ujinsia kuwa anayelima ni wa kike wakati
sentensi ya Kiswahili bado ilikuwa na swali kuwa anayelima ni mwanaume au
mwanamke. Hivyo lugha zote mbili yaani kiingereza na Kiswahili sarufi yake
inajitemea kama ilivyojidhihirisha katika mifano ya sentensi hapo juu
Kwa
ujumla kila lugha huwa na utaratibu na kanuni zake katika kupanga maneno na
kuunda sentensi na mpangilio, hii inaweza kukaribiana kwa lugha za jamii moja
kwa moja na pia ukatofautiana sana na lugha za jamii tofauti, kwa kuona kuwa
kila lugha huwa ina utaratibu wake na kanuni zake ni dhahiri. Hivyo lugha ya
Kiswahili inajitegemea katika sarufi yake na siyo inajiegemeza katika sarufi ya
kiingereza, kwani Kiswahili ni lugha inayojitoshereza kimaana a katika ubora
wake japokuwa ina ukaribu na lugha zingine kama kiingereza na kibantu pia.
USHAIRI WA ZAMA ZA ZILIPENDWA NA ZA SASA
B. F. KIWALE
P.O BOX 774
IRINGA
© Kiwale, F. Brasto 2016
ISBN 9976 911 59 1
chapa ya PILI 2016, January 2016.
Haki zote zimehifadhiwa. hakuna sehemu ya kazi hii itakayo ruhusiwa kuirudia kuitengeneza, kwa namna yoyote ile, bila ruhusa ya mwandishi au B. F Consult P.O. Box 774, IRINGA.
Printing and publishing consultancy by
KIWALE org/ TFC, P.O Box 327,
Iringa, Tanzania.
Ushairi
ni sanaa ya lugha inayoeleza jambo au wazo kwa njia ya mkato, na kwa namna
inayoleta hisia za msomaji au msikilizaji.
Maneno ya mashairi huteuliwa kimakusudi (ili yalete taswira maalum
akilini mwa msikilizaji au msomaji).
Maneno hayo pia hupangwa ili yatoe mdundo fulani shairi linapoimbwa,
linaposomwa au linapoghanwa (Njogu, 1999:87).
Kwa
ujumla, ushairi ni sanaa ya lugha inayotumia lugha ya mkato, maneno ya hekima,
lugha ya picha yenye mpangilio fulani wa vina na mizani unaovuta hisia za msomaji
au msikilizaji ili kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.
Muktadha wa utanzu
wa ushairi wa kiswahili katika kipengele cha fani umekuwa ukitumiwa na vipindi
vyote viwili yaani kipindi cha zama hizi na kipindi cha ushairi wa zilipendwa,
kwa namna tofautitofauti kupitia vipengele vifuatavyo;
Matumizi
ya lugha, katika muktadha wa utanzu wa ushairi wa kiswahili wa zama hizi; lugha
inayotumika ni rahisi na inayoeleweka kwa hadhira, kwa kuwa washairi wa sasa
hawafungwi na kanuni za ushairi wa kijadi. Kwa mfano, msanii Roma katika wimbo
wake wa “Mathematics” anasema
“…Nchi imeuzwa vigogo wanatuita ATM
Tuwakemee
mafisadi wote wa CCM…”
Hivyo kupitia
kipande hiki hadhira inapata ujumbe wa moja kwa moja wa ufisadi. Lakini ushairi katika zama za zilipendwa
lugha iliyokuwa inatumika ni ngumu kutokana na uthibiti wa tabaka tawala. Pia
uzuri wa ushairi wa kipindi hicho ulibainishwa kupitia lugha nzito, mfano
Shaaban Robert katika shairi la “Mtu na Malaika” anasema “…Wa huku hafiki huko, wala halina
malisho,
halishibishi kuchosha,
njiaye ina uchovu,
na tabu inayokwisha, wala
hupati utuvu… (Mlokozi, 1979:30).
Taswira,
katika zama hizi taswira zinatumika hususani katika suala la mapenzi kwa lengo
la kupendezesha kazi zao. Mfano Msanii
Ngwea katika wimbo wake wa “Kimya kimya” anasema; “…watu wanazamia hadi uchumvini…” akimaanisha watu wa
kileo wanafanya tendo la ndoa bila umakini.
Pia katika uchumi ushairi wa zama hizi umekuwa ukitumia taswira kwa
lengo la kuelimisha jamii mfano msanii Solo Thang katika wimbo wake wa “Miss
Tanzania” anasema “…Maliasili
ndo kitasa kila funguo, inapita…” Akimaanisha uwekezaji wa masharti
nafuu. Katika zama za kale/au mashairi ya zilipendwa yalitumia ujenzi wa
taswira kwa kurejelea vitu au mambo yaliyopendwa zaidi zama hizo, mfano wimbo wa Miriam makeba wa “malaika” ulitumika kujenga
taswira juu ya matendo ya mwanamke mwema kwa mumewe “...sina
neno mimi, kwa kuwa najua, penzi upepo
penzi maam… ipi siku…, penzi upepo, penzi
maua…”
msanii huyu anajenga taswira ya namna penzi
linavyoweza kunawili au kudhoofu kutokana
na linavyotunzwa kama ua liweze kunyauka au kustawi kutegemeana na
matunzo unayoyapata.
Muktadha wa
utanzu wa ushairi wa Kiswahili katika zama hizi na zilipendwa maudhui
yamejibainisha kwa namna tofautitofauti kupitia dhamira zifuatazo;
Suala
la utawala na uongozi, wasanii wa kipindi hiki wengi wao wamekuwa wakiwakosoa
moja kwa moja viongozi wanaoenda kinyume na taratibu za uongozi. Mfano Msanii
“Ney wa Mitego” katika wimbo wake wa “Salamu zao” anasema “…Ridhiwani mwambie dingi yako masela
hatumuelewi” Pia Roma katika wimbo wake wa “Mathematics” anasema ‘‘…mauti yangetufika bila kumpiga
Jakaya…” washairi wa kimapokeo waliandika wasifu wa viongozi wa zama
hizo, mfano, Katika utenzi wa “Fumo Lyongo” alitunga shairi la kumsifu mfalme, (Uk 13 ubet 13). “…Ni mwanamume Swahihi, kama simba una zihi...” Pia
Ottu Jaz Band wimbo wa “Naye Mwalimu Nyerere”(1970) wanasema “Naye mwalimu Nyerere jemedari wa
Afrika”
Suala
la mapenzi washairi wengi wa zama hizi wanazungumzia suala la mapenzi kwa kiasi
kikubwa zaidi ya asilimia 50 wanazungumzia mapenzi kwa sababu mapenzi yana soko
kubwa. Mfano Msanii Zay-B katika wimbo
wake wa “Ananitesa” anasema
“…Nakupenda
pia nakutaka pia..” Pia msanii K-Lynn na Bushoke katika wimbo wa “Machozi
ya fuaraha” wanasema “Mapenzi si
maneno, mapenzi ni vitendo”
pia katika zama za zilipendwa washairi
walizungumzia suala la mapenzi ili kuelimisha tu jamii lakini si kwa ajili ya
soko tu. Mfano katika utenzi wa Mwanakupona (Uk 112) ubeti 47 msanii anasema
“…ukae na mume wako…”
Suala
la utamaduni, washairi wa zama hizi baadhi yao hutweza utamatuni wao na
kuukweza utamaduni wa kigeni, mfano, Vanesa Mdee katika wimbo wake “Come over”
anasema “…Uliniomba namba nami
nikakataa! Oooh! I think about you baby” (Nakuwaza sana mpenzi). Hivyo
wapo baadhi wanaousifu utamaduni wao. Mfano.
Mr. Ebbo katika wimbo wa “Mimi Mmasai” uliopo katika albamu ya “Fahari yako”
anasema;
“…Mimi Mmasai bwana
nasema mimi Mmasai, tamaduni yenye nguvu iliyobaki Afrika…” Katika swala
la utamaduni wakati wa zama za zilizopendwa washairi walitunga kazi zao kwa
kutumia lugha zao kuusifu utamaduni wao. Mfano Shaaban Robert katika shairi la
“Titi la Mama” anasema;
“…Kiswahili
naazimu, sifayo iliyofumbwa…”
Pia katika
kipengele cha ujumbe katika ushairi wa zama hizi hutolewa katika kali ya uwazi
bila kificho mfano katika kitabu cha “Uzalendo” shairi la “Kweli iko wapi”? (uk.37) Msanii anasema
“…Cheche
ulipozitema, orodha ukisema,
mchafu asosafika, vipi lulu
kageuka?
Mshairi anamaanisha kuwa viongozi
wengi ni wanafiki katika kutoa maamuzi mfano, wapo tayari kuwapokea waovu kwa
maslahi binafsi. Katika zama za zilipendwa aghalabu ujumbe ulitolewa kwa uficho
huku mshairi akifikirisha zaidi hadhira, kwa sababu uzuri wa ushairi wa kipindi
hicho ulibainishwa kupitia lugha nzito.
Mfano Shaaban Robert katika shairi la Mtu na Malaika anasema “…wa
huku hafiki huko wala halina malisho…”
Hivyo basi, Kuna utofauti wa
muktadha wa ushairi wa Kiswahili wa kisasa na ule wa zama za zilipendwa, kwani
muktadha wa zilipendwa ulifungwa na sheia za vina na mizani, kwa sasa muktadha
wa ushairi wa sasa upo huru (hakuna sheria zinazombana) jambo lililopelekea
wasanii kuwa wengi kaibuka.
Subscribe to:
Posts (Atom)